Ngome ni nini?  Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?

Ngome ni nini?  Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?

Neno hili utaona likijuridia mara nyingi katika biblia husani katika maneno ya Daudi,  Kwamfano utaona katika  2Samweli 22:2  Daudi anasema… “.Bwana ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu, naam, wangu;

Kwanini amfananishe Bwana na Ngome, Je! Hii ngome ilikuwa ni ipi?

JIBU: Zamani karibu kila nchi au taifa kubwa lilikuwa ni lazima liwe na ngome. Hii ilijengwa, mahususi kwa lengo la kujificha dhidi ya maadui wanaotaka kuja kuharibu au kuteka au kuua, na ilijengwa ndani ya mji, kwa kuta ndefu sana na pana. Sehemu nyingine yalikuwa ni majengo makubwa yaliyojengwa kwa matofali mazito, kiasi kwamba hakuna namna yoyote adui anaweza kupanda au kuingia ndani ya kuta hizo kuharibu,.

Na juu kabisa ya kuta hizo, ngome nyingine ziliwekewa na  mInara ya walinzi kabisa, ambapo walinzi  walizunguka usiku na mchana kuangalia pande zote ni wapi  hatari inayotokea. Na kama wakiona maadui zao wanakuja, watu wote wa mji walikimbilia katika ngome hizo kujificha.

Tazama kwenye picha baadhi ya ngome za zamani zilivyokuwa;

ngome za zamani

Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolitaja neno hilo;

Zaburi 18:2 “Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu”.

Zaburi 71:3 “Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Nitakakokwenda sikuzote. Umeamuru niokolewe, Ndiwe genge langu na ngome yangu”.

Zaburi 144:2 “Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu”.

Soma pia. Zaburi 31:3, Yeremia 16:19

Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu,

Sasa mpaka hapo unaweza kupata picha ni nini Daudi alikuwa anamaanisha alipokuwa anamtaja Mungu  kama ngome yake.

JE NA SISI NGOME YETU NI NINI?

Hatuna ngome nyingine zaidi ya YESU KRISTO,. Hapa duniani hata uwe na nguvu nyingi kiasi gani, uwe ni maarufu kiasi gani, uwe na walinzi wengi kiasi gani, kama huna Kristo, huwezi kumshinda adui yako ibilisi kwa namna yoyote ile. Yesu  pekee ndiye anayeweza kuyaficha maisha ya mtu adui yeyote asiweze kuyadhuru,. Yesu ni kila kitu, ndio kiini cha maisha ya mwanadamu yeyote hapa duniani.

Yeye ndio mwamba, ndio jabali, ndio ngao, ndio kimbilio, ndio ngome, ndio kila kitu.. Tukisema kila kitu, maana yake ni kila kitu kweli, hata pumzi unayoivuta ni kwasababu ya neema  ya Yesu tu, ingekuwa sio yeye  usingekuwepo hata duniani.

Hivyo ndugu ikiwa wewe bado upo nje ya Kristo, ni wazi kuwa unajitenga na uhai wako mwenyewe tu. ni heri umkimbilie sasa ayaokoe maisha yako, Hizi ni nyakati za mwisho, hizi ni nyakati za hatari ambazo hazijawahi kutokea katika historia ya dunia, shetani anajua wakati wake ni mfupi, hivyo ameongeza bidii sana katika nyakati hizi za kumalizia, ili kukua wewe, ambaye bado huna ngome yoyote ya kujifichia..Sasa ikiwa kila siku unamkwepa Kristo, na huku ukidhani, kesho yako itakuwa salama kama leo, usijidanganye usijidanganye ndugu yangu.. Biblia inatuambia saa ya wokovu ni sasa.

Hivyo kama upo tayari leo, kutubu na kumpokea, ili afanyike NGOME imara ndani ya maisha yako kuanzia sasa, uamuzi huo utakuwa na busara sana kwako. Kama ni hivyo, fungua hapa kwa ajili ya sala ya toba na maelekezo mengine.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MWAMBA WETU.

BWANA HUWAJUA HAO WAMKIMBILIAO.

CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.

NITAFANYA YERUSALEMU KUWA JIWE LA KUWALEMEA .

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Dismas kiprotich limo
Dismas kiprotich limo
3 years ago

Hello