Wayebusi walikuwa ni “wana wa Kaanani”. Kujua Wakaana walikuwa ni watu gani unaweza kufungua hapa >> Wakaanani.
Lakini Watoto wa Kaanani ndio walikuwa hawa “Wayebusi”. Hivyo Wayebusi hawakuwa kabila kubwa, ukilinganisha na Kaanani, baba yao, na waliishi katika sehemu ndogo tu ya nchi ya Kaanani.
Mwanzo 10:15 “Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi, 16 na MYEBUSI, na Mwamori, na Mgirgashi ”.
Mwanzo 10:15 “Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
16 na MYEBUSI, na Mwamori, na Mgirgashi ”.
Wayebusi kama walivyokuwa Wakaanani na Wahivi, na Wahiti, walikuwa ni watu wanaoabudu miungu, na kufanya mambo ambayo yalikuwa ni machukizo mbele za Bwana, kwani walikuwa wanafanya uchawi, wanaloga, wanawapitisha wana wao kwenye moto kama sadaka kwa miungu yao n.k
Kumbukumbu 18:9 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. 14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo”.
Kumbukumbu 18:9 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.
10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.
14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo”.
Kutokana na machukizo hayo, Mungu aliwaondoa katika nchi ya Kaanani, kama alivyowaondoa wakaanani wenyewe Pamoja na Wahivi na Wahiti.
Lakini hata baada ya kuondolewa na Yoshua, walisalia wachache waliokaa katika baadhi ya miji..na mojawapo ya mji waliokuwa wanakaa ni Yerusalemu.
Yoshua 15:63 “Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo”.
Mji wa Yerusalemu hapo kwanza, kabla haujaitwa Yerusalemu, ulikuwa unaitwa YEBUSI, kufuatia jina la hawa Wayebusi, na ulikuwa unakaliwa na hawa Wayebusi, lakini baadaye kipindi cha wafalme, Daudi alikuja kuutwaa na kuwaondoa katika mji huo na kuuita Yerusalemu..
Waamuzi 19:10 “Lakini huyo mtu hakukubali kukaa usiku huo, ila akainuka, akaenda zake, akafika mkabala wa Yebusi (huo ndio Yerusalemu); nao walikuwako pamoja naye punda wawili waliotandikwa; suria yake naye alikuwa pamoja naye”.
2Samweli 5:6 “Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo”.
Jamii ya Wayebusi, sasa haipo tena, imepotea kabisa..Na Bwana ndiye aliyeipoteza, kutokana na Machukizo waliyokuwa wanayafanya!.
Na kama maandiko yanavyosema, Bwana Mungu ni yule yule, jana, leo na hata milele, habadiliki..Maana yake ni kwamba aliyokuwa anayachukia enzi hizo ndiyo anayoyachukia mpaka leo. Kama aliwatowesha Wayebusi na wakaanani, basi atawatowesha pia watu wafanyayo hayo, katika siku za mwisho.
Na nyakati hizi za mwisho, maasi yamekuwa makubwa kuliko hata waliokuwa wanayafanya Wayebusi na Wakaanani.
Hadi leo watu wanaua Watoto wao, (kwa kutoa mimba na kafara), hadi leo watu wanafanya uchawi na ushirikina n.k, mambo hayo ndio yanayotujulisha kuwa tunaishi katika siku za Mwisho, na ghadhabu ya Mungu inakaribia kumwagwa duniani kote.
Lakini hekima ya Mungu inatuonya tutoke katika vifungo vya dhambi, kwa kumpokea Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, na kubatizwa kwa jina lake na kwa Roho wake, ili tuokoke na ghadhabu ijayo.
Matendo 2:40 “Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”.
Maran atha
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Wakaanani walikuwa ni watu gani?
Wahiti ni watu gani?
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)
Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?.
Rudi nyumbani
Print this post