Ni eneo la pango ambalo lilikuwa karibu na mji wa Israeli unaoitwa Hebroni, ambalo Ibrahimu alilinunua kwa mtu mmoja aliyeitwa Efroni, kwa ajili ya maziko ya mke wake Sara.
Mwanzo 23:13 “Akamwambia Efroni, na watu wa nchi wanasikiliza, akisema, Tafadhali unisikilize; nitatoa kima cha shamba, nawe ukipokee kwangu, nami nitamzika humo maiti wangu.
14 Efroni akamjibu Ibrahimu, akamwambia,
15 Bwana wangu, unisikilize. Sehemu ya nchi, ambayo thamani yake ni shekeli za fedha mia nne, n’nini hii baina yako na yangu? Basi uzike maiti wako.
16 Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara”.
Eneo hilo baadaye lilikuja kugeuka kuwa kaburi la kifamilia, kwani hapo hapo ndipo Ibrahimu alipokuja kuzikwa na watoto wake, halikadhalika, ndipo Yakobo na Esau walipomzikia baba yako Isaka,
Na wakati wakiwa kule Misri, Yakobo aliwaagiza Watoto wake,pia wakamzike katika kaburi hilo la familia, la Makpela.
Mwanzo 49:29 “Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;
30 katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.
31 Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea;
32 shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi”.
Eneo hilo kwasasa, pale Israeli limejengwa msikiti, ujulikanao kama “msikiti wa Ibrahimi”, japo wote wayahudi na waislamu, hakuna hata mmoja anaweza kusema anao umiliki wa moja kwa moja wa hapo.
Lakini Je pango la makpela lina umuhimu kwetu hadi sasa au kwa Wayahudi?
Pango hili, au lolote lile ambalo lilizikiwa watakatifu, halina umuhimu wowote katika Imani yetu, Zaidi ya mambo ya kihistoria tu. Myahudi au mkristo yoyote ukizikwa karibu na eneo hilo, hakutakufanya uende mbinguni, Wapo wengine wanafikiri, wakienda Yerusalemu na kuomba kwenye ule ukuta wa Nehemia wa maombolezo, ndio maombi yao yatasikiwa. Au wakienda kubatizwa katika mto Yordani kama Bwana Yesu ndio ubatizo wao utapokelewa, jambo ambalo sio kweli.
Halikadhalika na Pango hilo la makpela halina umuhimu wowote, kwa mtu yeyote, kuzikiwa pale.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Watoto wa Ibrahimu/Wana wa Ibrahimu walikuwa ni wangapi?
Je! ni halali kwa mtu wa Mungu kutumia njia za uzazi wa mpango,ikiwamo mipira?
Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri.
About the author