Kaanani ni jina la zamani la nchi za Mashariki ya kati!..Eneo la Kaanani liliundwa na sehemu ya nchi zifuatazo, Nchi ya Israeli yote, pande za Magharibi mwa nchi ya Yordani, Kusini mwa nchi ya Lebanoni na nchi ya Palestina yote.
Nchi ya Kaanani, hapo kwanza ilikuwa inakaliwa na watu waliojulikana kama Wakaanani, ambao biblia inawataja kama watu waliokuwa wenye sifa na wenye maumbile makubwa. Ndio maana tunasoma kipindi wale wapelelezi wa Kiisraeli walipotumwa kuipeleleza nchi hiyo ya Kaanani, walirudi na ripoti ya kuogopesha, wakasema wamekutana na Wanefili ndani ya hiyo nchi.
Hesabu 13:31 “Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, HATUWEZI KUPANDA TUPIGANE NA WATU HAWA; KWA MAANA WANA NGUVU KULIKO SISI.
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; NA WATU WOTE TULIOWAONA NDANI YAKE NI WATU WAREFU MNO.
33 KISHA, HUKO TULIWAONA WANEFILI, WANA WA ANAKI, WALIOTOKA KWA HAO WANEFILI; TUKAJIONA NAFSI ZETU KUWA KAMA MAPANZI; nao ndivyo walivyotuona sisi”.
Nchi ya Kaanani Mungu alimpa Ibrahimu na uzao wake wote, Ndio maana Wakaanani waliokuwa wanaishi katika nchi hiyo (Hao wanefili) Mungu alikuja kuwaondoa kwa mkono hodari..
Mwanzo 17:7 “Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao”
Baada ya Israeli kuitwaa Sehemu ya nchi ya Kaanani, waliibadilisha jina na kuiita Nchi ya Israeli. Na tangu wakati huo mpaka leo, inajulikana kama nchi ya Israeli, Ingawa si sehemu yote, sehemu nyingine ya Kaanani, Mungu hakumalizia kuwapa wana wa Israeli, kwasababu walikengeuka na kuanza kuingia maagano na wakaanani.
Waamuzi 2:1 “Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi;
2 nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?
3 Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu
4 Ikawa, hapo huyo malaika wa Bwana alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia”
Kiroho, safari ya wana wa Israeli, kutoka Misri kwenda Kaanani, inafananishwa na safari yetu sisi ya kwenda Mbinguni (kwenye nchi yetu ya Ahadi) kutoka katika Ulimwengu wa dhambi.
Na kama jinsi safari ile ilivyokuwa na Majaribu mengi njiani, kiasi kwamba walioanza Safari kuanzia mwanzo hadi mwisho walikuwa ni wachache sana, yaani watu wawili tu (Yoshua na Kalebu). Vivyo hivyo safari ya kwenda mbinguni ni mapambano, kwasababu watakuwa wachache sana watakaoshinda…
Luka 13:22 “Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu. 23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”
Hapo anasema TUJITAHITI!!..maana yake ni kwamba “JITIHADA BINAFSI PIA ZINAHITAJIKA” .. Si suala la kukaa tu na kuomba na kusubiri!…bali ni suala la kutia bidii pia!!…Wengi watakaoikosa mbingu ni kwasababu ya kutotia bidii kuutafuta ufalme wa Mungu!..(maana yake ni watu wasio na jitihada katika mambo ya kiMungu).
Sasa swali ni je!, mimi na wewe tunazo hizo jitihada za kuingia katika Kaanani yetu?.
Kama bado upo nje ya Wokovu, (yaani hujampokea Yesu) basi fahamu kuwa upo katika hatari ya kuikosa mbingu na kama tayari umeshampokea Bwana Yesu lakini unaishi maisha ya uvuguvugu, ya kutokujali, ya kusukumwa sukumwa, au kumbembelezwa bembelezwa…basi fahamu kuwa upo mbali na ufalme wa mbinguni, na siku ya kurudi kwa Bwana itakukuta kama mwivi.. kwasababu maandiko yanasema “tutie jitihada”.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
Biblia ilimaanisha nini watu wasitoe vizazi vyao kwa Moleki?
Kwanini iwe ni nchi ibubujikayo maziwa na asali?
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
About the author