Swali: Katika 1Petro 2:13 Tumeambiwa tutii kila kitu tunachoamriwa na wafalme, lakini katika Matendo 5:29, tunaona Petro huyo huyo hawatii wenye mamlaka, anasema imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu..Je hapo panakaaje?
Jibu:Tusome
1 Petro 2:13 “Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;14 ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema”
1 Petro 2:13 “Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;
14 ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema”
Tusome tena…
Matendo 5:29 “Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”.
Ni kweli tumeamriwa kutii mambo yote, lakini si hata yale yasiyofaa. Kwamfano inatokea mkuu wa nchi au mwenye mamlaka anatoa amri ya watu kuabudu kitu fulani ambacho si Mungu wa mbingu na nchi (yaani Yehova).. Hapo hatuwezi kumtii, kwasababu kavuka mipaka, au mkuu anatoa amri hakuna kuhubiri injili, au kuomba au kufunga, hapo tumepewa ruhusa ya kutotii maagizo yake hayo.
Lakini mambo mengine, ambayo hayaathiri imani yetu, hayo hatuna budi kutii..
Kwamfano sheria imetolewa na wakuu wa nchi kuwa siku fulani itakuwa ni siku ya usafi nchi nzima, kwamba watu wote watoke wafanye usafi, hapo hatuna budi kutii, kwasababu jambo hilo haliathiri imani yetu, na zaidi sana litatuongezea ushuhuda mzuri katika jamii na linafaa kwa afya zetu. Na sheria nyingine zote mfano wa hizo, hatuna budi kuzitii.
Lakini ikitoka sheria ya kutukataza kumwabudu Mungu, au sheria ya kutulazimisha kufanya mabaya, sheria hiyo tumepewa ruhusa ya kuivunja, na tukawa hatujafanya dhambi, bali kinyume chake tukawa tumempendeza Mungu.
Ndio maana Petro ijapokuwa alilihubiri suala hilo la kuwatii wenye mamlaka, (Katika hiyo 1Petro 2:13) lakini ilipofika wakati hao wenye mamlaka walipowakataza wasihubiri habari njema za ufalme wa mbinguni… Petro na Yohana hawakukubaliana na hiyo sheria..ndipo wakasema imewapasa kumtii Mungu kuliko wanadamu, wakisaidiwa na Malaika wa Mungu.
Matendo ya Mitume 5:18 “wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;19 lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema20 Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.21 Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.25 Mtu mmoja akaja akawapasha habari ya kwamba, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu.26 Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe.27 Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza,28 akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”.
Matendo ya Mitume 5:18 “wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;
19 lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema
20 Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.
21 Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.
25 Mtu mmoja akaja akawapasha habari ya kwamba, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu.
26 Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe.
27 Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza,
28 akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.
29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”.
Na sio tu kwa wafalme na wenye mamlaka, tuliopewa ruhusa ya kuvunja amri zao zilizozidi mipaka, bali hata katika familia..endapo Mume katoa sheria ya mke au watoto kuabudu miungu, hapo tumepewa ruhusa ya kutomtii mzazi huyo au mume kwa agizo hilo..Kwasababu ni agizo lililovuka mipaka..
Mathayo 10:37 “Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili”.
Lakini mume akitoa amri au sheria ambazo haziathiri imani zetu, hizo hatuna budi kuzitii, mfano mzazi anatoa amri ya kufanya shughuli fulani ya nyumbani iliyo halali hapo hatuna budi kutii hata kama hatutaki..
Kwahiyo kwa ufupi tumepewa amri ya kutii yote yaliyo mema lakini hatujapewa amri ya kutii mambo mabaya. Lakini yote hatuna budi kuyafanya kwa hekima.
Bwana atusaidie.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312.
Mada Nyinginezo:
JE NI KUTII AU KUPATA KWANZA MAARIFA?
KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU.
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Nini maana ya vifungeni viuno vya Nia zenu? (1Petro 1:13).
MIMI NI ALFA NA OMEGA.
Rudi nyumbani
Print this post