Jina kuu la Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana lihimidiwe!. Karibu tujifunze biblia.
Je unajua maana ya kuzaliwa mara ya pili kwa Neno?.. Kupo kuzaliwa mara ya pili kwa maneno ya watu au ya mtu na pia kupo kuzaliwa mara ya pili kwa Neno la Mungu.
Neno la Mungu linasema hivi…
Yohana 3:3 “ Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU”.
Yohana 3:3 “ Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU”.
Umeona tafsiri ya kuzaliwa mara ya Pili kwa Neno la Mungu ni ipi?…si nyingine zaidi ya KUZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO.
Sasa unaweza kujiuliza maana ya kuzaliwa kwa maji na kwa roho ni nini?
Kuzaliwa kwa maji ni “Ubatizo wa Maji mengi”, na kuzaliwa kwa roho ni “Ubatizo wa Roho Mtakatifu” Kwahiyo unapoamini na kubatizwa kwa Maji tele (Yohana 3:23).. Na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, basi hapo unakuwa umezaliwa mara ya Pili kwa NENO LA MUNGU…(Kwasababu Neno la Mungu ndio linaelekeza hivyo).
Sasa umuhimu wa kufanya hivyo ni nini?
Ukiamini na kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, faida yake ya kwanza ni kwamba WOKOVU WAKO UNAKUWA NI WA KUDUMU, unakuwa sio wa kuchafuka chafuka..bali unakuwa ni thabiti siku zote mpaka siku utakapomaliza maisha yako hapa duniani.. Kwasababu Neno la MUNGU ni mbegu isiyoharibika.. Hivyo ukizaliwa kwa Neno la Mungu hilo (yaani kwa kubatizwa kwa maji na kupokea Roho mtakatifu), basi wokovu wako unakuwa imara daima…Ndivyo Neno la Mungu linavyosema..
1Petro 1:23 “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si KWA MBEGU IHARIBIKAYO, BALI KWA ILE ISIYOHARIBIKA; KWA NENO LA MUNGU LENYE UZIMA, lidumulo hata milele”
Ni kwanini leo wokovu wa watu wengi unakuwa ni wa kusuasua, unakuta mtu leo kamkiri Yesu, lakini baada ya siku kadhaa au wiki kadhaa karudi kule kule, ijapokuwa yupo kanisani na karibu na wapendwa?.. ni kwasababu huenda mtu huyo hajazaliwa mara ya pili kwa Neno la Mungu (yaani kwa kubatizwa sahihi na kupokea Roho Mtakatifu)…
Huenda baada ya kumkiri Yesu akaambiwa hakuna haja ya ubatizo, au akakawishwa kubatizwa! Na kupokea Roho Mtakatifu… Hivyo kwa mbegu hiyo aliyopandikiziwa ndani yake, hawezi kusonga mbele kwasababu ni MBEGU INAYOHARIBIKA.. Lakini kama angezaliwa mara ya pili kwa Neno la Mungu, ambalo ndio mbegu isiyoweza kuharibika basi wokovu wake ungekuwa ni imara siku zote.
Ndugu unayesoma ujumbe huu, huenda wokovu wako ni wa nusu nusu, kiasi kwamba hata wewe mwenyewe hujielewi kama Kweli Kristo yupo ndani yako au la!.. katika hali hiyo uliyopo hebu jichunguze kama kweli umezaliwa katika Neno la Mungu.. Kwasababu Neno la Mungu linasema “Ni lazima kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho”.
Je! Wewe umebatizwa inavyopaswa?.. kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa maji tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Bwana Yesu Kristo (Matendo 2:38)..Na ubatizo sahihi wa Roho Mtakatifu ni ule unaozaa matunda yale yaliyoorodheshwa kwenye Wagalatia 5:22. Kama vitu hivyo viwili umevikosa, basi ni vizuri ukatafuta ubatizo sahihi haraka iwezekanikavyo na vile vile ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Ikiwa mahali ulipo unaweza kupata ubatizo sahihi basi anza kwenda kuutafuta kuanzia sasa, lakini ikiwa unapata ugumu katika kutafuta, basi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba zetu hapo chini, tutakusaidia kukuelekeza mahali karibu na ulipo, ambapo utaweza kupata ubatizo sahihi.
Bwana Yesu akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.
Mkomamanga ni nini? Na katika biblia unawakilisha nini?
TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
Rudi nyumbani
Print this post