USIIKARIBIE DHAMBI, KAA NAYO MBALI.

USIIKARIBIE DHAMBI, KAA NAYO MBALI.

Je unajua kwamba kuikaribia dhambi ni “DHAMBI”, Hata tu kabla ya kuifanya?.

Mungu hakumpa tu Adamu maagizo ya kutokula yale matunda ya mti wa katikati…bali  pia alimwambia “Asiyaguse yale matunda”..asije akafa. Wengi wetu tunaona tu habari ya “kula” kama kosa, lakini hatujui kuwa  Mungu aliwaagiza kwamba hata kuyagusa wasiyaguse, (maana yake wakae mbali nayo).

Mwanzo 3:2 “Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;

3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala MSIYAGUSE, msije mkafa”.

Kumbe hata wangeyagusa tu yale matunda bila hata ya kuyala, bado Wangekufa!!.

Hii ni hatari sana..na inatupa fundisho kubwa sana..

Kwanini Mungu akataze wasiyaguse?..Je kuna ubaya wowote katika kuyagusa???… Jibu ni ndio!… kwasababu chanzo cha dhambi ya kula tunda ni kulishika lile tunda kwanza, (Hawa asingeweza kulipeleka mdomoni kabla ya kulishika) kabla ya kulichunguza chunguza kwanza, kabla ya kulidadisi dadisi, ndipo akaangukia katika ushawishi wa kulila.

Hivyo Mungu aliona chanzo cha dhambi kuwa ni “kushika” ndipo akatoa maagizo kwamba WASIYAGUSE!! Wasije wakafa… lakini wenyewe (Waligusa, na tena wakala) Hivyo ikawa ni makosa mawili yaliyozaa Mauti kamilifu.

Na hata leo Bwana anatuonya tukae mbali na dhambi, tusiikaribie kabisa dhambi, tusiiguse dhambi licha ya kuitenda!!..

Tukae mbali na Wizi kama ya wizi wenyewe kutendeka,…tukae mbali na  Ulevi kabla ya ulevi wenyewe kutendeka… tukae mbali na Utukanaji, Uadui, Kiburi, Uasherati, kabla ya kufanya mambo hayo (Wagalatia 5:19-20)… Tusizikaribie kabisa hizi dhambi!!.. tukae nazo mbali maili nyingi sana, kwasababu kitendo cha kuzikaribia tu tayari ni kosa..

leo hii utaona mtu anasema  hazini, wala hafanyi uasherati lakini katika simu yake kumejaa picha zinazochochea mambo hayo, kumejaa miziki inayochochoea mambo hayo, kumejaa filamu zi kidunia zenye maudhui hayo ya kiasherati, simu yake imejaa magroup ya mizaha, na uhuni, unaochochea mambo hayo…pasipo kujua kuwa anafanya makosa makubwa kuisogelea dhambi kwa namna hiyo..

Neno la Mungu linasema kwamba tuikimbie zinaa, sio tuishi nayo, au tuikemee!..bali tuikimbie (Soma 1Wakorintho 6:18 )...kama vile Yusufu alivyoikimbia mbele ya mke wa Potifa, na sisi tunapaswa tuikimbia hivyo hivyo Yusufu hata hakukubali kuzungumza na Yule mwanamke..

Lakini ni kinyume chake katika siku hizi za mwisho, utaona binti anayekiri kumpokea Yesu anapiga maneno na mwanaume anayemtaka, kijana anayekiri kumpokea Yesu anapiga maneno ya kidunia na binti anayemtamani, na hata kufanya naye mizaha..Hii ni hatari kubwa!, kumbuka ushawishi wa Hawa kula tunda haukuanzia mdomoni bali mkononi!..baada ya kulishika ndipo ushawishi ukamwingia..

Na sisi tukijishikamanisha na dhambi, basi ni lazima tutazitenda tu!, haijalishi itachukua muda gani ni lazima tutazitenda tu!…Hauwezi kusema umeacha utukanaji, lakini kila kukicha kampani zako ni za watu wanaotukana…ni lazima tu na wewe utatukana, haijalishi itakuchukua muda gani kudumu bila kutukana lakini mwisho wa siku utaishia kurudia matukano tu.

Hauwezi kukaa unasikiliza usengenyaji na wewe usiwe msengenyaji..ni suala la muda tu!, utajikuta na wewe upo kama wao.. Kumbuka Adamu na Hawa waliambiwa “wasiukaribie kabisa ule mti, na hata kuugusa”.. Vile vile na sisi leo hii tunapaswa tusiikaribie miti ya dhambi…wala tusiguse mashina yake wala matawi yake.. maana kugusa ndio chanzo cha kula..

Bwana atusaidie na kutuwezesha katika yote.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

MUME / MKE BORA KUTOKA KWA BWANA UTAMWONA UKIWA KATIKA MAZINGIRA GANI?

HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO

FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.

Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana,

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Matendo mwandaza elie
Matendo mwandaza elie
1 year ago

Asante sana kwa neema ya mungu ambayo bado anawa aciya watu wake ku okoka kila mahali maneno yake ameiweka ili kuwa fikiya wote walio gizani, na mungu awape nyote mlio fanyikisha maneno haya ku eneya pote ku mu ona siku ya mwisho wa mambo yote

Amos
Amos
1 year ago

Mbarikiwe sana watumishi wa Mungu. Sikujutia kwa kujoin na kundi hili makini, naamini Mungu amewapa neema ya tofauti mno na azidi Kuwapa kibali ili kuufikia ulimwengu….