Kwanini maombi kwa Marehemu si sahihi kibiblia?

Kwanini maombi kwa Marehemu si sahihi kibiblia?

Jibu: Katika biblia hakuna mahali popote panapoonyesha marehemu waliombewa..isipokuwa katika sehemu moja tu inaonyesha Marehemu mmoja aliyekuwepo katika mateso ya kuzimu aliomba ndugu zake walio hai wakahubiriwe injili ili wasife katika dhambi na kwenda kule aliko, lakini tunaona maombi yake hayo hayakuwa na matokeo yoyote.
Hebu tuisome hiyo habari..

Luka 16:27 “Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishiwa hata na mtu akifufuka katika wafu”

Umeona?..Huyu Tajiri alijaribu kuwaombea watu walio hai wasifike alipo lakini maombi yake yalizuiliwa, halikadhalika Sisi tulio hai hatuwezi kuwaombea watu waliokufa kwamba watolewe katika mateso ya kuzimu.

Kama kuna maombi ya kuwaombea wafu watoke katika mateso ya kuzimu na kuingia paradiso, basi vile vile yatakuwepo pia maombi au sala za kuwatoa watu peponi na kuwapeleka kuzimu.. Lakini kama hakuna maombi ya mtu kumtoa mtu peponi(yaani paradiso) na kumpeleka kuzimu…vile vile hakuna maombi yoyote ya kuweza kumtoa mtu kuzimu na kumpeleka peponi.

Utasema tunazidi kulithibitisha vipi hilo kimaandiko?

Hebu tuzidi kuisoma hiyo habari ya Tajiri na Lazaro…Tuangalie maombi mengine aliyoomba kuhusiana na yeye kutolewa kule.

Luka 16:23 “Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ILI WALE WATAKAO KUTOKA HUKU KWENDA KWENU WASIWEZE; WALA WATU WA KWENU WASIVUKE KUJA KWETU”.

Hapo mwisho anasema..kati Yao (hao walio kuzimu na walio peponi)..KUMEWEKWA SHIMO KUBWA kama mpaka, ili walio kuzimu wasiweze kuvuka kuingia peponi na walio peponi wasivuke kwenda kuzimu..Ikiwa na maana kuwa hakuna mwingiliano wowote wa walio kuzimu na walio peponi..Hilo shimo katikati yao lipo mpaka sasa.

Hivyo kwa hitimisho, maombi ya kuwaombea heri Marehemu au kuwaombea wapunguziwe adhabu ni maombi yasiyo ya kimaandiko na hayana matokeo yoyote… Vile vile sala za kuwaomba watakatifu waliofariki watuombee halipo kimaandiko.

Ni vizuri kutengeneza maisha yetu hapa duniani kabla ya kufa, kwa kumwamini Bwana Yesu na kutubu dhambi, kwasababu tukishakufa hakutakuwa na nafasi nyingine ya pili.

Yohana 8:24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”.
Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je sisi wakristo tunaruhusiwa kufanya 40 za marehemu?

MATESO YA KUZIMU.

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?

USIRUHUSU INZI WATUE JUU YA ROHO YAKO.

JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments