Masomo maalumu kwa watumishi wa Mungu (Wahubiri).
Je umebeba ushuhuda gani katika injili yako?.
Tujifunze jambo kwa Yohana Mbatizaji..
Yohana 10:40 “Akaenda zake tena ng’ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko. 41 Na watu wengi wakamwendea, wakasema, yohana kweli hakufanya ishara yo yote, LAKINI YOTE ALIYOYASEMA YOHANA KATIKA HABARI ZAKE HUYU YALIKUWA KWELI. 42 Nao wengi wakamwamini huko”.
Yohana 10:40 “Akaenda zake tena ng’ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko.
41 Na watu wengi wakamwendea, wakasema, yohana kweli hakufanya ishara yo yote, LAKINI YOTE ALIYOYASEMA YOHANA KATIKA HABARI ZAKE HUYU YALIKUWA KWELI.
42 Nao wengi wakamwamini huko”.
Hapo maandiko yanasema Yohana hakufanya ishara yoyote kama alivyofanya Musa katika hatua ya kuwahubiria ukombozi wana wa Israeli, au kama alivyofanya Eliya aliposhusha moto, au kama alivyofanya Eliya na manabii wengine..
Lakini Yohana yeye tunasona alibeba kitu kingine cha ziada.. Na kitu hicho ni “USHUHUDA WA KWELI WA YESU”. Na ndicho kilichomfanya aonekane mbele za Mungu kuwa mkuu kuliko manabii wote waliotangulia..
Mathayo 11:9 “Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na ALIYE MKUU ZAIDI YA NABII.…… 11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa WANAWAKE ALIYE MKUU KULIKO YOHANA MBATIZAJI; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye”.
Mathayo 11:9 “Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na ALIYE MKUU ZAIDI YA NABII.……
11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa WANAWAKE ALIYE MKUU KULIKO YOHANA MBATIZAJI; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye”.
Kwahiyo kumbe kinachojalisha si miujiza?, si ishara, si maajabu tunayoyatenda.. bali ni kile tunachokihubiri kumhusu Yesu?.. Je kina ukweli?.. na kama kina ukweli, je ni katika kiwango gani?
Yohana alianza kuhubiri habari za Toba na ondoleo la dhambi na kusema Ufalme wa Mungu umekaribia wamwamini yeye ajaye.
Mathayo 3:1 “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, 2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Mathayo 3:1 “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,
2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Injili ya namna hii ndiyo Bwana Yesu aliyoanza kuihubiri pia…
Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Umeona injili ya Yohana iliyovyofanana na ya Bwana?..Yohana aliuona ushuhuda wa Yesu na akauhubiri kabla hajaja, aliona hizi ni nyakati za kutubu na kumrudia Mungu, kwasababu ufalme wa Mungu umekaribia!!.. .
Vile vile hakuanza kuwaambia watu watubu halafu baadaye waendelee na dhambi zao, bali aliwaambia watubu na baada ya hapo wazae matunda yapatanayo na toba zao, wala wasijisifie dini, wala madhehebu.. Maana yake baada ya kutubia uzinzi ni lazima waishi maisha ya usafi baada ya hapo, kama umetubia ulevi ni lazima wauache ulevi, kama wametubia ukahaba ni lazima wauache ukahaba na vifaa vyote vya ukahaba, ikiwemo mavazi!..(hiyo ndio maana ya kuzaa matunda yapatanayo na toba).
Luka 3:7 “Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? 8 Basi, TOENI MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. 9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; BASI KILA MTI USIOZAA MATUNDA MAZURI HUKATWA NA KUTUPWA MOTONI”.
Luka 3:7 “Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?
8 Basi, TOENI MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.
9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; BASI KILA MTI USIOZAA MATUNDA MAZURI HUKATWA NA KUTUPWA MOTONI”.
Injili ya namna hii ndiyo iliyobarikiwa na Bwana Yesu, na ndiyo iliyochaguliwa kuwa NJIA KWAAJILI YA BWANA!, Na ndiyo iliyomfanya Yohana awe mkuu kuliko manabii wote ingawa hakufanya muujiza wowote.
Je! Na wewe kama mtumishi wa Mungu unahubiri nini? Je unahubiri mambo ya ulimwengu huu au injili ya ufalme wa Mbinguni??.. Injili yako ni ya magari na majumba na pesa?..
Kumbuka Injili ya ufalme wa mbinguni ni ile ile haijabadilika ambayo ni “kutubu na kuzaa matunda yapatanayo na toba kwamaana ufalme wa mbinguni umekaribia” Huo ndio ushuhuda wa Yesu na ndio roho ya unabii.
Ufunuo 19:10b “….. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii”.
Vile vile usikimbilia kutafuta au kutengeneza miujiza, usitumie nguvu nyingi kutafuta maajabu… bali tafuta kwanza Ushuhuda wa Yesu, ukiupata huo utakuwa umepata muujiza mkubwa sana katika utumishi wako!.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU
WAKO WATATU WASHUHUDIAO MBINGUNI NA DUNIANI.
IJUE HEKIMA YA MUNGU KATIKA KUKUINUA KIMAISHA.
JE UMEKUFA PAMOJA NA NANI?
Rudi nyumbani
Print this post