NIFANYE NINI ILI NISILALE NINAPOSOMA BIBLIA.

NIFANYE NINI ILI NISILALE NINAPOSOMA BIBLIA.

Mara nyingi tunapojikuta tumelala tunaposoma biblia, huwa moja kwa moja tunamsingizia shetani. Lakini ukweli ni kwamba shetani anahusika kwa sehemu ndogo, sehemu kubwa ni hali zetu za kimwili ndio zinakuwa adui katika jambo hili. Mazingira ambayo ni mashambulizi kutoka kwa adui mfano wake yanakuwa ni  kama haya; pengine mtu akianza tu kusoma biblia anasikia maumivu makali kwenye kichwa, au mwili, lakini akiacha tu kusoma hali yake inarudia kama kawaida, au anaona giza au vitu kama mianga mianga kwenye macho na hivyo inamfanya asiweze kuisoma biblia, au kila anapotaka kusoma anapoteza hapo hapo kumbukumbu zote kwamba alikuwa anasoma biblia, na hatimaye anajikuta yupo usingizini, au anafanya mambo mengine kabisa, hiyo ndio mfano ya mashambulizi.. Na inahitaji kuombewa, au kushindana na hiyo roho hadi ikutoke.

Lakini ukijiona unaposoma biblia usingizi mzito umekukamata, unasinzia sinzia, unapiga piga miayo, huyo sio adui huo ni mwili wako, usiopenda mambo ya rohoni. Hivyo ni lazima uushinde huo.

Wagalatia 5:17  “Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka”

Hivyo hizi ni njia ambazo zitakusaidia usilale pale unaposoma biblia.

1) Omba kabla ya kusoma biblia

Usipende kufungua biblia kama kitabu cha riwaya, unasoma tu utakavyo. Kumbuka yale ni maneno ya ROHO, na hivyo inahitaji umkaribishe Roho akusaidie. Hivyo  usiwe mvivu wa kuomba, pata dakika, kadhaa za kufanya hivyo. Ni jambo ambalo nimejifunza sana, wakati nasoma biblia bila kuomba, na pale ninapoomba kisha nikaisoma, kuna tofauti kubwa sana ya kiuelewa na kiutulivu. Maombi pia yanasaidia kama kuna mashambulizi yoyote, basi yanatowekea hapo.

2) Pata muda wa kupumzika.

Ikiwa umechoka sana, si lazima usome biblia muda huo huo. Pendelea kuruhusu mwili wako upumzike vizuri, kwamfano umetoka kazini, umeshughulika kutwa nzima, ni rahisi sana kukabwa na usingizi muda huo huo usomapo biblia peke yako. Hivyo tumia busara, wahi kulala, kisha amka usiku. Ukilala hata masaa 3, mwili unapokea taarifa kuwa huyu mtu tayari alishapumzika. Hivyo ukiamka ukajimwagia maji, ukaketi utajiona unafuu mkubwa, na utapata kitu kikubwa kuliko kulizimisha mwili wakati umechoka.

3) Usipende kusomea biblia kitandani:

Tafuta meza ukae, mwili wako uwe kama mtu aliye darasani, sio kama aliye hospitalini mgonjwa unasubiriwa kuhudumiwa. Kaa kwenye meza, kisha ndio usome biblia yako

Luka 12:35  Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka

4) Kuwa na daftari na kalamu.

Kusoma kwa kuandika na kwa sauti, huwa kuna matokeo makubwa kuliko, kutumia tu macho yako. Hivyo andiko vifungu unavyovisoma, na ufunuo unaopata, itakuongezea umakini katika usomaji wako, na hivyo Roho Mtakatifu atapata nafasi ya kukufindisha kwa urahisi zaidi.

5) Soma na wengine.

Ukiona huwezi kujiwekea ustaarabu wa kuzingatia ratiba yako ya usomaji, pendelea kujifunza na wengine. Kaa na familia yako, au ndugu zako, au rafiki yako katika Bwana jiwekeeni ratiba ya usomaji wa biblia pamoja, kisha mnachambua kile mlichojifunza, kwa namna hiyo itakusaidia sana kuielewa ..

Mathayo 18:20  “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao”

 6) Soma kwa vituo.

Kusoma biblia sio mashindano kwamba ni lazima uimalize yote kwa siku moja, soma vifungu kadhaa, kisha tumia muda mwingi, kuvitafakari hivyo vilimaanisha nini. Roho Mtakatifu anapenda kutufundisha taratibu sana, hataki tuvuke madarasa ya juu wakati ya chini bado hatujayamaliza. Hivyo zingatia kusoma kwa muktadha wa kuelemishwa na Roho Mtakatifu, sio kumaliza silabasi. Kusoma vifungu vitano kwa dakika mbili, kisha ukavifakari kwa masaa 2, ni bora kuliko kusoma vifungu elfu kwa saa2, halafu hakuna tafakari yoyote.

7) Mifungo

Mfungo ni jambo zuri ambalo huupa mwili wepesi, kwasababu mwili unapotaabika kwa kunyimwa haja zake kwa kawaida roho yako huwa inakuja juu. Hivyo ukiwa katika kipindi cha mfungo, utaona wepesi Fulani wa kuisoma biblia kwa masafa marefu kidogo, kuliko kipindi kingine. Fungu mara kwa mara, au ukiwa unatamani wiki hiyo kuitumia vizuri usiku katika kusoma Biblia, basi hakikisha wiki hiyo yote unafunga, utajiona mwepesi sana hususani wakati wa usiku unapotulia.

8) Mshirikishe mkufunzi wako

Si kila jambo utaweza kulitatua tu peke yako mengine, utahitaji msaada, hivyo hakikisha maendeleo yako ya kiusomaji, kiongozi wako anayafahamu, hatua zako unamshirikisha mchungaji wako, itakusaidia sana, kupata ushauri au maombi , au ushuhuda kwa yale ambayo pengine usingeyafahamu uwapo peke yako. Na hiyo itakupa hamasa zaidi na shauku ya kusoma.

Bwana akubariki.

Hakikisha unasoma BIBLIA kila siku.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Jinsi ya kuandaa Somo la kufundisha

JINSI YA KUSOMA BIBLIA.

Tirshatha ni nini? (Ezra 2:63)

HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?

UFUNUO NI NINI, NA NITAPOKEAJE UFUNUO KUTOKA KWA MUNGU?

Biblia inamaana gani inaposema tutoapo unabii tutoe kwa kadiri ya imani?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments