Maana ya Mithali 19:15 ‘Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;

Maana ya Mithali 19:15 ‘Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;

Fahamu Maana ya Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”.


Mara nyingi Sulemani kwa hekima ya Roho aliongozwa kuona uhusiano uliopo kati ya uvivu na umaskini. Kama tu kinyume chake, sehemu nyingine alivyoweka uhusiano kati ya bidii na utajiri(Mithali 10:4). Vivyo hivyo uvivu na umaskini havipishani.

Na kama anavyosema hapo, uvivu humpeleka mtu katika usingizi, lakini sio usingizi tu bali ule mzito, Kwasababu gani? Ni kwasababu mwili haupo katika hali ya kujishughulisha, na hivyo utalala tu, na Bado utaendelea kulala siku baada ya siku.. Na matokeo yake kutokuzalisha chochote kinachoonekana, hatimaye, umaskini unaingia.

Hivyo mstari huo unalenga Nyanja mbili. Ya kwanza ni ule uvivu wa mwilini, na ya pili ni ule uvivu wa rohoni.

Uvivu wa mwilini:

Mungu katuumbia kufanya kazi, watu wote (ikiwemo watakatifu). Maana yake ni kuwa ikiwa huna huduma yoyote ya madhabahuni Bwana amekuitia, ambayo inakufanya utumike muda wote hapo. Ni sharti ufanye kazi. Mtume Paulo alilionya kanisa juu ya watu ambao hawafanyi kazi kwamba ni sharti wajishughulishe ili wapate na kitu cha kuwagawia na wengine (2Wathesalonike 3:10)

Uvuvu wa rohoni:

Lakini pia Uvuvi wa rohoni. Mtakatifu anapokuwa mvivu, kusoma Neno, yaani muda wa Neno anakwenda kutazama filamu, anakwenda kijiweni kucheza drafti,.Anakuwa  mvivu kuomba, Unapofika huo muda tu anaona usingizi ni bora kuliko kuomba,.Au Mtakatifu hataki kushuhudia habari za Kristo kwa wengine, anasema jua kali. Sasa mtu huyo anajiandaa kuwa maskini kiroho. Yaani atakuwa katika wokovu usiokuwa na matunda, ukuaji wake wa kiroho utakuwa hafifu, Neema ya Mungu haitatenda kazi kwa wingi juu yake, na hivyo atakosa mema mengi ya Mungu katika safari yake wa wokovu hapa duniani.

Uvuvi wowote, una hasara, kwahiyo tuuweke katika orodha ya maadui zetu wa imani.

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?

Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni  ipi?

SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!

Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments