Maganjo kibiblia? (Walawi 26:31)

Maganjo kibiblia? (Walawi 26:31)

Jibu: Tusome,

Ganjo” ni mahali palipoharibika.. Jengo lililoharibika linaitwa “Ganjo” yakiwa mengi yanaitwa “maganjo”, mji ulioharibiwa aidha kwa vita au kwa janga fulani pia unaitwa “Ganjo”.

Katika biblia neno hili limeonekana mara kadhaa..

Walawi 26:30 “Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia. 

31 Nami nitaifanya MIJI YENU IWE MAGANJO, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo. 

32 Nami nitaitia hiyo nchi ukiwa; na adui zenu watakaokaa huko wataistaajabia”

Tusome pia…

Ezekieli 29:12 “Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, ITAKUWA MAGANJO muda wa miaka arobaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.”

Neno hili pia unaweza kulisoma katika mistari ifuatayo likiwa na maana hiyo hiyo..Walawi 26:33, 2Nyakati 34:6, Ayubu 3:14, Isaya 6:11, 7:19, Yeremia 4:7, Ezekieli 6:14, 36:38, na Amosi 9:14.

Vile vile hii dunia siku moja itafanyika kuwa “GANJO”, kutokana na dhambi!.. Bwana ataiharibu kwa moto kama alivyoiharibu nyakati za Nuhu, kwa maji.

2Petro 3:6 “kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.

7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu”.

Je umeokoka? Kama bado, saa ya wokovu ni sasa, tupo mwisho wa nyakati.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?

Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa?

Kama Malkia Esta alijipamba je! Kuna ubaya gani wanawake wa wakikristo wa leo kujipamba?.

TAA YA MWILI NI JICHO,

VICHEKESHO NA UTANI MADHABAHUNI

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments