Karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu lililo Taa ya njia yetu na Mwanga wa Njia zetu (Zab 119:105).
Je sisi wanadamu tunaweza kuufanya Moyo wa Mungu uwaelekee watu wengine?. Jibu ni Ndio!. Katika biblia kuna watu baadhi ambao kwa sehemu waliweza kuufanya Moyo wa Mungu uwaelekee watu wake, ijapokuwa watu hao hawakustahili kabisa kukaribiwa na Mungu.
Na watu hawa wi wengine Zaidi ya NABII MUSA NA NABII SAMWELI
Hebu tuweke msingi kwa kutafakari maandiko yafuatayo…
Yeremia 15:1 “Ndipo Bwana akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu MUSA na SAMWELI, MOYO WANGU USINGEWAELEKEA WATU HAWA; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao”.
Kumbe Musa na Samweli walikuwa wanatabia ya kuuelekeza Moyo wa Mungu kwa watu wake?.. Sasa kwa namna gani?…hebu tusome matukio yao baadhi, mmoja baada ya mwingine.
1. MUSA.
Kutoka 32:7 “Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao,
8 wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.
9 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu
10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
11 MUSA AKAMSIHI SANA BWANA, MUNGU WAKE, NA KUSEMA, BWANA, KWA NINI HASIRA ZAKO KUWAKA JUU YA WATU WAKO ULIOWALETA KUTOKA NCHI YA MISRI KWA UWEZA MKUU, NA KWA MKONO WENYE NGUVU?
12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.
14 NA BWANA AKAUGHAIRI ULE UOVU ALIOSEMA YA KWAMBA ATAWATENDA WATU WAKE”.
Hapo Mstari wa 14 unasema, Bwana akaghairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake. Na hiyo yote ni baada ya Musa kuwaombea wana wa Israeli, na hivyo Mungu akaghairi yale mabaya nakuendelea kutembea na watu wake.
Huenda Musa asingewaombea basi wote wangefutiliwa mbali na kweli Mungu angeenda kumfanya Musa kuwa Taifa kuu.
Lakini si huyo tu peke yake, tumwangwalie na Samweli pia.
2. SAMWELI
1Samweli 12:16 “Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, Bwana atakalolitenda mbele ya macho yenu.
17 Leo je! Si mavuno ya ngano? Nitamwomba Bwana, kwamba apeleke ngurumo na mvua; NANYI MTAJUA NA KUONA YA KUWA UOVU WENU NI MWINGI SANA, MLIOUFANYA MACHONI PA BWANA, KWA KUJITAKIA MFALME.
18 Basi Samweli akamwomba Bwana, naye Bwana akapeleka ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa Bwana sana, na Samweli pia.
19 Watu wote wakamwambia Samweli, Utuombee sisi watumwa wako kwa Bwana, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.
20 Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata Bwana, bali mtumikieni Bwana kwa mioyo yenu yote.
21 Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili,
22 visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.
23 WALAKINI MIMI, HASHA! NISIMTENDE BWANA DHAMBI KWA KUACHA KUWAOMBEA NINYI; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka”
Hapo mstari wa 23, Nabii Samweli anawaombea wana wa Israeli kwa Bwana, ambao kimsingi walikuwa wanaenda kuangamizwa kutokana na dhambi yao ya kujitakia mfalme, lakini Samweli anasimama kuwaombea na kuwaambia maneno ya faraja.
Je na sisi tunawaombea wengine na kuwapatanisha na Mungu wao kama alivyofanya Musa na Samweli?
Huenda hasira ya Mungu imewaka juu ya kanisa la Mungu, je! Unasimama kuliombea?, huenda hasira ya Mungu imewaka juu ya familia yako, je unasimama kuiombea toba?..huenda hasira ya Mungu imewaka juu ya ndugu zako, juu ya jamii yako, juu ya nchi yako, juu ya watu wengine.. Je unasimama kuwombea? Au unawahukumu na kuwalaumu?.
Bwana atusaidie tuwe watu wa kuwaombea wengine na kuwapatanisha na Mungu wao, na hata ifikie hatua ya kuona kuwa “KUTOWAOMBEA WENGINE NI DHAMBI”, na hapo tutafananishwa kama wana wa Mungu. Kumbuka siku zote kuwa Mungu anatumia watu, na hivyo katika wokovu wa wengine anatafuta mtu atakayeweza kusimama mahali palipoboka ili asimwage hasira yake, na mtu huyo ni mimi na wewe, ikiwa tutakuwa tayari kutumiwa na yeye.
Mathayo 5:9 “Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu”.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
NIFANYE NINI NIWEZE KUDHIBITI HASIRA?
About the author