Kuota unakata kucha.

Kuota unakata kucha.

Nini tafsiri ya kuota “unakata kucha”

Swali: Niliota nipo kanisani na mimi ndio bibi-arusi, na mchungaji akaniambia nitoke nikakate kucha ndio nirudi kufunga ndoa, nini tafsiri yake?

Jibu: Tusome mistari ifuatayo.

Kumbukumbu 21:10 “Utakapokwenda vitani kupigana juu ya adui zako, na Bwana, Mungu wako, awatiapo mikononi mwako, nawe uwachukuapo mateka,

11 ukaona kati ya mateka mwanamke mzuri, ukafanya tamaa kwake, ukawaza kumtwaa kuwa mkeo;

12 ndipo umchukue kwenu nyumbani kwako, naye atanyoa kichwa, AKATE NA KUCHA

13 avue na mavazi ya uteka wake akae nyumbani mwako, awakalie matanga babaye na mamaye mwezi mzima, kisha uingie kwake uwe mumewe, naye awe mkeo.”

Kucha ndefu za mkononi ni ishara ya “uteka”. Mwanamke aliyetekwa katika vita zamani, kabla ya kuolewa na wale waliomteka ilikuwa ni sharti wamnyoe nywele na kumkata kucha!. Lengo la kufanya vile ni kuondoa ufahamu wa maisha ya kwanza, na kumweka katika ufahamu wa maisha mapya.. ambapo kiroho ni kama anaondolewa roho ya uteka ndani yake, na kuingizwa roho ya uhuru katika jamii mpya anayoenda kuianza.

Kwahiyo kama wewe ni mwanamke, na umeota mchungaji amekwambia ukakate kucha ndipo urudi ufunge ndoa ,tafsiri yake ni kwamba kuna vifungo umefungwa ambavyo ni lazima vifunguliwe kwanza ndipo uweze kuingia katika ndoa!.

Ni kifungo kikubwa na cha kwanza ndani ya maisha ya mtu ni “dhambi”. Biblia inasema “atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi” (Yohana 8:34).

Kwahiyo ni lazima ujiangalie maisha yako na ufikiri kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha, na pia kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo ili upate ondoleo la dhambi zako (Matendo 2:38) na pia kupokea Roho Mtakatifu. Kwa kufanya hivyo utakuwa umewekwa huru mbali na kifungo cha dhambi na vifungo vingine vya roho na mwili.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba kucha ndefu ni ishara ya utumwa wa dhambi, hivyo zingatia kuokoka kikweli kweli, kabla ya kufanya mambo mengine yoyote, usijivunie dini wala dhehebu, bali okoka na simama.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Kuota unasubiriwa mahali fulani uhutubie, halafu unachelewa.

Kuota upo nchi nyingine.

KUOTA UNAOLEWA/UNAOA.

KUOTA UNATOKA DAMU YA HEDHI.

KUOTA UNAKOJOA KITANDANI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments