Nini maana ya “Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake” (Isaya 9:6)?.

Nini maana ya “Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake” (Isaya 9:6)?.

Jibu: Turejee Isaya 9:6,

Isaya 9:6 “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; NA UWEZA WA KIFALME UTAKUWA BEGANI MWAKE; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani”.

Katika jeshi lolote lile, liwe la Ulinzi au la wananchi, kunakuwa na vyeo.  Si askari wote wanafanana kimadaraka, wapo wenye madaraka makubwa na wapo wenye madaraka madogo. Na utaona ili kumtofautisha askari mmoja na mwingine kimadaraka, wanakuwa na sare ambazo zina alama Mabegani mwao, alama hizo ni maarufu kama “Nyota”.

Sasa nyota zile mabegani si ‘urembo’ bali zinafunua mamlaka Fulani/cheo cha yule askari.. ndio utaona wale wenye nyota nyingi basi wanakukuwa na Vyeo vikubwa Zaidi na mamlaka makubwa Zaidi.

Kwamfano utaona “Jenerali wa Jeshi” ndiye mtu mwenye cheo kikubwa Zaidi katika jeshi, na mara nyingi anakuwa ameshapitia ngazi zote za chini kama Ukoplo, Brigedia Jenerali, meja-Jenerali, au luteni-Jenerali.

Na mpaka amefikia ngazi hiyo ya Ujenerali, maana yake ndiyo ngazi ya juu na hakuna nyingine. Na anatofuatishwa na Askari mwingine si kwa sura, jinsia au kimo, bali anatofautishwa na “ule uwezo uliopo begani mwake” (yaani zile nyota nne begani mwake). Askari wengine waonapo zile nyota mabegani basi watapiga saluti na kutii..

Sasa serikali nyingi za kidunia zimenakili baadhi ya mambo kutoka katika Serikali iliyo juu (yaani ya mbinguni).

Kama yupo Jenerali wa jeshi la wanadamu, vile vile yupo JENERALI MKUU WA JESHI LA MBINGUNI, na huyo si mwingine Zaidi ya BWANA YESU KRISTO!. Ambaye ana nyota zi kifalme begani mwake, nazo ndizo hizo zilizotajwa (MSHAURI WA AJABU, na MUNGU MWENYE NGUVU, na BABA WA MILELE na MFALME WA AMANI).

Hiyo ndio maana biblia inamtaja BWANA YESU KRISTO kama BWANA WA VITA, na MFALME WA WAFALME, Kwasababu yeye ni Jenerali Mkuu.

Ufunuo 17:14  “Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu”.

YESU pekee ndiye njia ya  UZIMA, na Bwana wa vita, na Mfalme wa Wafalme, ambaye hana wa kulinganishwa naye, kwasababu ndiye mwenye mamlaka yote ya mbinguni na duniani (Mathayo 28:18).

Je umemwamini Huyu Mkuu (YESU)?.. Je bado hujaona tu kuwa hakuna wokovu kwa mwingine yoyote isipokuwa yeye?..bado hujaona tu kuwa hakuna mwenye nguvu nyingi Zaidi yake yeye?.

Yeye pekee yake ndiye mwenye uwezo wa kufungua na kufunga, leo hii kama utampokea Basi atakufungua katika vifungo vya dhambi na mizigo yote ya adui shetani (Mathayo 11:28), vile vile atakufungua na vifungo vyote vinavyokutesa, kwasababu Bega lake linahubiri UWEZA MKUU.

Isaya 22:22 “Na ufunguo wa nyumba ya DAUDI NITAUWEKA BEGANI MWAKE; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.”

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mikononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?

Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?

Swali: Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.

Je ni kweli hakuna aliyepaa mbinguni zaidi ya Mwana wa Adamu? (Yohana 3:13)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments