Isaya 40:12 ‘maji kwa konzi ya mkono, na mbingu kwa shubiri’

Isaya 40:12 ‘maji kwa konzi ya mkono, na mbingu kwa shubiri’

SWALI: Naomba kufahamu nini maana ya Isaya 40:12 inaposema maji kwa konzi ya mkono, na mbingu kwa shubiri?

Isaya 40:12 “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani”?


 JIBU: Ukianzia kusoma vifungu vya juu na kuendelea vile vya chini, utaona Mungu anawaambia watu wake Israeli kuwa atawajilia kama mchungaji awachungaye kondoo wake , na kuwalisha, na kuwakuongoza, na kuwakusanya kifuani mwake, hata wale walio wachanga, ndivyo atakavyowatendea watu wake na hilo litawezekana.

Lakini Israeli waliona kama jambo hilo linaweza lisiwe rahisi, Ndio hapo akawaambia sasa katika vifungu vifuatavyo maneno hayo. Kwamba “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake”? Maji anayoyazungumzia hapo ni maji mengi, mfano wa bahari, na maziwa Je! Kuna mtu yeyote anayeweza kuyakusanya maji mengi namna hiyo kwenye viganja vyake? Jibu ni hapana! Lakini kwa Mungu ni jambo dogo sana.

Vilevile anawauliza ni nani awezaye ‘kuzikadiri mbingu kwa shubiri’?. Shubiri ni kipimo cha urefu, wa kiganja, toka kidole gumba mpaka kile cha katikati vinaponyooshwa. Na ni wazi hakuna mtu anayeweza kupima ukubwa wa mbingu, toka sayari moja hadi sayari nyingine, kwa kipimo chochote kile cha kibinadamu. Lakini kwa Mungu hilo ni jambo dogo sana, ni kama kuzipima kwa shubiri.

Halikadhalika anauliza  ni nani awezaye kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi?. Pishi ni kopo dogo, je kuna mwanadamu anaweza kuyakusanya mavumbi yote duniani, kama vile akusanyavyo yale machache kwenye kopo lake. Ni wazi hakuna awezaye kuwa na pipa la uwezo huo.

Vilevile anauliza ni nani anayeweza kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?. Je! Kuna mizani yoyote ya kibinadamu inaweza kuiweka milima juu yake, na kutoa vipimo?. Jibu ni hakuna. Lakini kwa Mungu ni jambo dogo sana. Milima ni kama vipunje vidogo sana vya mchanga.

Ikiwa haya yanaonekana magumu kwa mwanadamu, lakini kwa Mungu ni mepesi. Vivyo hivyo jambo la kuwakusanya watu wake, au kuwasaidia, lisitizamwe kibinadamu, kwasababu uweza wa Mungu ni mkuu sana usioweza kufikirika kibinadamu. Maswali ya namna hii ndio kama yale Mungu aliyokuwa anamuuliza Ayubu, (Ayubu 38-41), na katika Mithali 30:4

Yesu kama mchungaji wetu mkuu, anauwezo wa kutukusanya kama kondoo wake. Haijalishi tutaonekana tumetawanyika mbali kiasi gani, lakini akisema jambo ni lazima liwe. Halikadhalika na katika mambo yetu yote ya kiroho na kimwili.

Hivyo kitabu cha Isaya sura ya 40 yote, kinaeleza uweza wa Mungu, usiopomika kibinadamu. Lakini Swali ni Je! Kristo amekusamehe dhambi zako? Kama ni la! Basi nafasi bado unayo leo. Mwamini yeye akuokoe. Na kukupa ondoleo la dhambi zako.

Kwa mwongozo wa namna ya kupokea wokovu basi fungua hapa>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Nini maana ya mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe? (Mathayo 24:35).

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)

Kuna Mbingu ngapi?

Mbinguni ni sehemu gani?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments