Nini maana ya 1Wakorintho 4:7?

Nini maana ya 1Wakorintho 4:7?

SWALI: Naomba kufahamu maana ya 1Wakorintho 4: 7 

Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?


JIBU: Ukianza kusoma tokea sura ya kwanza utaona Paulo, anakemea sana baadhi ya tabia ya matengano ambayo ilionekana katika kanisa hili la wakorintho. Iliyozuka kutokana na aina ya mafundisho au utendaji kazi wa waasisi wa huduma, au waliowabatiza, na sana sana kati ya Paulo na Apolo.

Hivyo matabaka haya yakawafanya wajivunue wanadamu, na mafundisho yao. Bila kufahamu kuwa kanisa ni la Kristo na si la wanadamu.

Ndipo Paulo, akaweka wazi kuwa kila mmoja aliitwa kwenye utumishi wa Kristo Yesu, ambao una mchango wake katika kanisa, lakini si kwamba huduma ya mmoja ni bora kuliko nyingine. Akasema mmoja anapanda mwingine anatia maji, lakini mkuzaji ni Mungu.

Sasa katika vifungu hivi anaendelea kuwaambia tabia ya kupambanua watumishi, au huduma, si sawa.  Ndio hapo anasema “Nawe una nini usichokipokea?. Akiwa na maana je! Kuna kipawa gani, au kitu gani chema katika kanisa ambacho hawakukipokea kutoka kwa Mungu,?

Lakini anasema..

Iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?. Yaani kama vyote vilitoka kwa Mungu na sio kwa wanadamu, mbona basi mnajisifia kana kwamba vimekuja kwa uweza wa kibinadamu?.

Kama tumepewa kwa neema iweje sasa tujisifie, kana kwamba tumevipokea kwa nguvu zetu na utashi wa watumishi wetu, na ukuu wao, na uwezo wao wa kuhubiri vizuri? Karama hizi za rohoni hakuna hata mmoja imetoka kwa mwanadamu, wenyewe wamefanyika vyote tu. Hivyo wa kujivunia hapo na kusifiwa hapo ni Mungu wala si Paulo au Apolo.

Jambo ambalo hata leo huonekana kwa baadhi ya watu wa kanisa la leo. Ikiwa tuna msingi katika Kristo, iweje kujivunia makanisa au huduma, na kujiona sisi ndio bora zaidi ya wale wengine?

Ni kweli zipo huduma ambazo si za kweli, hazina msingi sahihi wa Kristo Yesu. Lakini ikiwa wote Injili yetu ni ya Kristo aliyesulubiwa kutukomboa sisi, basi tofauti za kiutendaji kazi, au kiujuzi, zisitufanye tujione bora, kwasababu sio hao wanadamu walitoa hivyo vipawa bali ni Roho Mtakatifu. Na anatenda kazi kama apendavyo yeye, anampa huyu hiki, anampa Yule kile.

Mmoja atapanda, mwingine atatia maji, mwingine mbolea, mwingine mvunaji, lakini atakuzaye ni Mungu mmoja, katika shina la Yesu Kristo Bwana wetu.

Kama mkristo ukijiona una vita vya kiuhuduma, ujue bado ni mchanga kiroho, bado unatabia za mwilini.

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?

FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.

MAUMIVU  NYUMA-YA-HUDUMA.

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

MBINGUNI YUPO NANI SASA?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments