Antiokia ni wapi kwasasa?

Antiokia ni wapi kwasasa?

Antiokia ipo nchi gani kwa sasa? Na nini tunaweza kujifunza kupitia mji huo?


Jibu: Antiokia ni mji uliopo kusini mwa Taifa la UTURUKI na Kaskazini mwa Taifa la SIRIA.

Mji huu una historia kubwa sana ya kanisa, kwani ndicho kitovu cha jina “Ukristo”. Maandiko yanasema Wanafunzi (yaani watu waliomwamini YESU na kumfuata) waliitwa “wakristo” kwanza hapo Antiokia na si Yerusalemu kanisa lilipoanzia.

Matendo 11:26  “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. NA WANAFUNZI WALIITWA WAKRISTO KWANZA HAPO ANTIOKIA.

27  Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia”.

Antiokia ni mji uliomiminiwa uliokuwa na Neema ya Ukristo kuliko miji mingi, lililojaa Mitume, manabii na waalimu.. kwani hata Mtume Paulo safari yake ya kuanza kuhubiri injili ilianzia pale.

Matendo 13:1 “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli.

2  Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.

3  Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

4  Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro”.

Matendo 14:26 “Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza”.

Mji wa Antiokia kwasasa umejaa wa Islamu kutokana na Taifa hilo la Uturuki kuwa la kiislamu, ingawa kuna asilimia ndogo ya wakristo wanaoishi humo. Mahali ambapo uamsho mkubwa wa injili ulianzia sasa adui kapateka na kupafanya kuwa mji wa kipagani… Na miji mingine imenyanyuka yenye uamsho kuliko huo, sawasawa na Neno lile..

Marko 10:31 “Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza”

Hivyo hiyo ni tahadhari hata kwetu, “Tushike tulicho nacho, mpaka mwisho adui asije akatupokonya taji yetu”.

Mji wa Antiokia mwaka 2023, Februari 6 kulitokea tetemeko kubwa sana lililoua watu elfu 55, na kuharibu makazi mengi sana.

Bwana atusaidie tuwe na mwisho mwema.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Yerusalemu ni nini?

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

MJI WENYE MISINGI.

Babeli ni nchi gani kwasasa?

DANIELI: Mlango wa 8

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Davis Hermans
Davis Hermans
6 months ago

Thanks for the words