Kemoshi ni nani? (Yeremia 48:46)

Kemoshi ni nani? (Yeremia 48:46)

Swali: Huyu Kemoshi alikuwa nani, na nini tunajifunza kutoka kwake?


Jibu: Turejee,

Yeremia 48:46 “Ole wako! Ee Moabu, Watu wa Kemoshi wamepotea; Maana wana wako wamechukuliwa mateka, Na binti zako wamekwenda utumwani”.

“kemoshi” hakuwa mtu bali alikuwa ni “mungu” wa watu wa Moabu. Kumbuka kila taifa lilikuwa na mungu wake; Israeli walikuwa na MUNGU wao ambaye ni YEHOVA, Muumba wa mbingu na nchi, Tiro walikuwa na mungu wao anayeitwa “baali”, Sidoni walikuwa na mungu wao anayeitwa “ashtoreti”, wana wa Amoni walikuwa na mungu wao anayeitwa “milkomu”. N.k na hawa wana wa Moabu mungu wao ndio anayekuwa anaitwa “kemoshi” ambaye kiuhalisia ni “pepo”.

Sasa utaona Mungu aliwakataza wana wa Israeli wasiabudu miungu mingine tofauti na yeye…lakini wapo waliotii na wapo waliokaidi na kuamua kuifuata miungu hiyo ya mataifa mengine na kuiabudu na kuisujudia. Na Mfalme Sulemani alikuwa miongoni mwa waliokengeuka dakika za mwisho kwa kuifuata miungu hiyo ya mataifa, ingawa baadaye alikuja kutubu.

2Wafalme 23:13 “Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, MFALME WA ISRAELI, KWA ASHTORETHI, CHUKIZO LA WASIDONI, NA KEMOSHI, CHUKIZO LA MOABU, NA MILKOMU, CHUKIZO LA WANA WA AMONI, mfalme akapanajisi”.

Hii miungu hata leo inaabudiwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo Africa, isipokuwa katika majina mengine tofauti na hayo.

Mila nyingi za kiafrica asili yake ni miungu hii, kwamfano mungu wa wasidoni aliyeitwa Ashtorethi alikuwa ni mtu wenye kuchongwa maumbile ya mtu, na kusujudiwa, na kufanyiwa matambiko..na sasa jamii nyingi na makabila mengi (ikiwemo na wakristo) wanafanya hayo hayo wanapokutanika katika vijiji vyao, pasipo kujua kuwa ni ibada za sanamu kama zile zile tu ambazo mataifa wasiomjua Mungu walikuwa wanazifanya.

Bwana atusaidie tuepukane na ibada hizo za sanamu.

Mistari mingine inayomtaja huyo mungu “kemoshi” ni pamoja na Hesabu 21:9, Waamuzi 11:24, 1Wafalme 11:7, 1Wafalme 11:33, Yeremia 48:7, na Yeremia 48:13.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Moabu ni nchi gani kwasasa?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?

MNGOJEE BWANA

USIJITUMAINISHE JUU YA SIRA YAKO ANGALI UPO KATIKA DHAMBI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments