Machukizo ni nini?

Machukizo ni nini?

Machukizo au Chukizo ni nini? kama tunavyosoma katika biblia?


Machukizo linatokana na neno “chukizo” na chukizo ni kitu kinachosababisha chuki/hasira. Kwa Mungu kitu chochote kinachoipandisha ghadhabu yake kinaitwa “chukizo”.

Na vitu vifuatavyo ndivyo vilivyokuwa machukizo kwa MUNGU.

   1. Ibada ya Sanamu.

Sanamu ya aina yoyote ile ilikuwa ni machukizo kwa Mungu na hicho ndicho kitu cha kwanza kilichokuwa kinaletea wivu kwa Mungu.

Kumbukumbu 27:15 “Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina”.

Kumbukumbu 32:16 “Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo.

17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa”.

Soma pia Kumbukumbu 27:15, na 2Wafalme 23:24

   2. Uasherati na ulawiti.

Walawi 18: 22 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo”.

Soma tena Mambo ya Walawi 20:13

   3. Mavazi yasiyopasa.

Kumbukumbu 22:5 “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”

Mfano wa mavazi yasiyopasa, ni suruali kwa mwanamke, na nguo mfano wa magauni kwa wanaume.

   4. Sadaka yenye kasoro.

Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.

Kumbukumbu 17:1 “Usimchinjie Bwana, Mungu wako, ng’ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.

Na yapo machukizo mengine mengi!.

Lakini pia lipo chukizo moja KUU na KUBWA ambalo litatokea kule YERUSALEMU, ambalo ni CHUKIZO LA UHARIBIFU, linalomhusu Mpinga-kristo.

Kwa upana juu ya CHUKIZO LA UHARIBIFU, basi fungua hapa >>CHUKIZO LA UHARIBIFU

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

VIPIMO MBALIMBALI VYA KIBIBLIA.

Kemoshi ni nani? (Yeremia 48:46)

Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?

Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments