Yeremia 48:11 “MOABU AMESTAREHE TANGU UJANA WAKE, NAYE AMETULIA JUU YA SIRA ZAKE, WALA HAKUMIMINWA KUTOKA CHOMBO KIMOJA KUTIWA CHOMBO KINGINE, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika. 12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Yeremia 48:11 “MOABU AMESTAREHE TANGU UJANA WAKE, NAYE AMETULIA JUU YA SIRA ZAKE, WALA HAKUMIMINWA KUTOKA CHOMBO KIMOJA KUTIWA CHOMBO KINGINE, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Unajua sira ni nini?
Sira ni yale makapi yanayosalia baada ya pombe kuchachushwa, ni mchanganyiko wa maganda ya mbegu na wadudu waliokuwa wanaichachusha pombe hiyo. Kwa kawaida pombe kama divai inapomalizika kuchachushwa, wanachofanya ni kuimimina kwenye vyombo vingine kwa ajili ya matumizi na kuiacha Sira chini.. kwasababu yenyewe inakuwa kama topetope au urojo urojo fulani hivi.
Lakini makapi haya huwa yanathamani kubwa sana kwa wachachushaji, kwasababu pombe inayokaa muda mrefu juu ya Sira, huwa inaubora tofauti na ile ambayo, imekaa kwa muda mfupi. Kwa jinsi itakavyokaa sana juu ya sira basi ladha ya divai ndivyo inavyokuwa nzuri sana, vilevile mwonekano wake na harufu yake inakuja Zaidi, Lakini ile ambayo imechachushwa tu na saa hiyo hiyo au baada ya kipindi kifupi ikaondolewa na kupelekwa katika vyombo vingine huwa haina uzuri saa kama ile iliyodumu muda mrefu juu ya sira.
Wanaotengeneza divai, za ghali kama vile zinazoitwa champagne, huwa zinaachwa muda mrefu juu ya sira, hata miezi 4 na Zaidi, hivyo ubora wake unakuwa wa juu Zaidi kulinganisha na divai nyingine za kawaida. (Soma pia Isaya 25:6)
Sasa tukirudi katika mstari huo tuliousoma hapo juu, biblia inasema..
“Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine…”
Moabu katika historia ni taifa ambalo, tangu lilipozaliwa halikupitia migogoro kabisa, au kama lilipitia basi ni midogo midogo sana ambayo haikulisababishia taifa hilo madhara makubwa, ukilinganisha na mataifa mengine, Moabu haikuwa na majanga, wala vita, wala njaa wala shida shida, lakini pamoja na kwamba ilijaliwa hivyo haikujua ni kwanini Mungu aliwaacha wawe vile, kinyume chake yenyewe iliendelea tu kufanya maovu na matendo yasiyompendeza Mungu kwa muda mrefu.
Na ndio maana hapo inafananishwa na divai ambayo imekaa juu ya sira yake kwa muda mrefu, divai ambayo haikuharakishwa kumiminwa miminwa kwenye vyombo vingine, ikiwa na maana kuwa haikuchukuliwa utumwani, haikupitishwa katika matatizo, iliendelea kubakia katika ustawi wake kwa muda mrefu..
Ikawa inadhani kuwa kamwe haitakaa ukumbane na mabaya, yenyewe imebarikiwa tu, ikafikiria hao wengine wanaoadhibiwa kama Israeli wana laaana na mikosi kutoka kwa Mungu.
Lakini tukisoma mistari inayofuata inasema hivi..
Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika. 12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
Umeona, kuna wakati ulifika, wakaldayo walikuja na kuwaangamiza na kuwachukua utumwani na kuwaharibu kabisa, na uzuri wao ukapotea ghafla, jambo ambalo hawakutazamia kama lingekaa liwapate, kama wengine.
Ndugu yangu, leo hii unatenda dhambi lakini huoni chochote, unazini Bwana hakuadhibu kwa lolote, unafanya mambo yako machafu kwa muda mrefu sasa, unakwenda kwa waganga, hauumwi, kinyume chake unazidi kustawi, unaendelea kufanya anasa na ulevu, unasema mbona hakuna dhara lolote linalonipata, hujiulizi ni kwa nini? Unachodhani ni kuwa wewe ni spesheli sana kwake sio? embu soma mstari huu tena ujifunze jambo..
Sefania 1:12 “Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami NITAWAADHIBU WATU WALIOGANDA JUU YA SIRA ZAO; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya”.
Umeona, Mungu utafika wakati atakuchunguza kwa taa, wewe ambaye umetulia juu ya Sira yako, huangaishwi angaishwi, unafanikiwa angali upo katika dhambi, unayesema, Mungu hawezi fanya jambo lolote hata nikiwa mwovu kiasi gani.
Jiangalie, hukumu ipo, utakufa ghafla, na moja kwa moja utajikuta upo jehanamu kama yule Tajiri wa Lazaro, ambaye hapa duniani alikuwa akijitumaisha katika Maisha yake ya anasa tu, hajali kama kuna kuzimu, au hukumu, hajali kama kuna kiama chake mbeleni.. Na wewe ndipo utakapojikuta huko kama hutatubu, ukilia na kuomboleza, ukisema laiti ningelijua, laiti ningelijua..
Wakati huo utakuwa umeshachelewa ndugu. Leo hii ukiona Mungu hafanyi chochote juu ya dhambi zako, sio kwamba anayafurahia hayo Maisha unayoishi, anakutazama tu, yamkini siku moja utatubu, lakini ikifikia wakati haoni badiliko lolote la wewe kumgeukia yeye, atakujia na kukuondoa duniani kama alivyofanya kwa Wamoabu.
Biblia inasema saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubali ni leo, usingojee siku Fulani ukasema hiyo ndio itakuwa siku yako ya wokovu, haitakaa ije kamwe. Mpe Yesu Kristo Maisha yako leo ayaokoe, Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha tafuta mahali ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO ili upate ondoleo la dhambi zako, na Kisha mwenyewe Mungu atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu ili akae na wewe siku zote za Maisha yako.
Hata kama ikitokea Maisha yako yamefikia ukingo leo, basi unaouhakika wa kuurithi uzima wa milele.
Ikiwa utapenda kuokoka, na unahitaji msaada huo basi unaweza, kutafuta kanisa la kiroho lililokaribu na wewe, wakusaidie au ukawasiliana na sisi kwa namba zetu hizi +255693036618 /+255789001312 kwa ajili ya Sala ya Toba na maagizo mengine.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
JE! ULEVI NI DHAMBI?.
“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?
KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.
Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 au saa 6?
UFUNUO: Mlango wa 15
Rudi nyumbani
Print this post