Swali: Kuna nini katika Divai mpaka Bwana YESU ayageuze maji kuwa Divai?
Jibu: Hakukuwa na chochote maalumu au cha kipekee katika Divai.
Sababu ya Bwana YESU kuyageuza maji kuwa Divai na si kinywaji kingine ni kwasababu ndicho kinywaji kilichokuwa kimepunguka pale! (Kulingana na zile taarifa alizoletewa na mama yake).. Endapo kama ingekuwa ni chakula ndicho kilichopunguka basi Bwana YESU angefanya muujiza wa chakula kuongezeka cha kuutosha ule umati wote, huenda angefanya muujiza kama ile ya Mikate na Samaki, alipolisha maelfu ya watu. (Marko 6:38-44 na Luka 9:13-17).
Sasa kabla ya kuangalia ni ujumbe gani tunapata kwa mwujiza ule, hebu kwanza tuangalie matokeo ya kukosa Divai katika ile Harusi.
Kufahamu kwa kina matumizi ya Divai katika biblia fungua hapa >>MATUMIZI YA DIVAI.
Kulingana na Desturi za kiyahudi ilikuwa ni aibu kubwa sana arusi ikose Divai, au chakula…Hivyo ni aibu kubwa sana kwa wanafamilia, sawasawa tu sasa sherehe ikipungukiwa na chakula inakuwa ni aibu kubwa kwa walioandaa na huzuni na karaha!..
Sasa kitendo cha Bwana YESU kubadili yale maji na kuwa Divai, tena yenye kuwatosha watu wote ni kitendo KILICHOWAONDOLEWA AIBU WANA ARUSI NA WAZAZI.. vile vile ni kitendo kilichowaondolewa huzuni, na masononeko na fadhaa.. na ni kitendo kilichowapa heshima. Ndio maana utaona yule mkuu wa Meza alimfuata Bwana arusi kumsifu badala ya Bwana YESU.
Sasa ni ujumbe gani mkuu tunaupata hapo?
Ujumbe mkuu si upekee wa Divai.. bali ni Faida ya BWANA YESU ndani yetu au katikati yetu. Kuwa yeye anapoingia ndani yetu anazichukua aibu zetu, na fadhaa zetu na masikitiko yetu, na kutuheshimisha na kutuondolea aibu zetu..
Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Unauona upendo wa YESU kwetu pale tunapomkaribisha na kumtwika fadhaa zetu?.. Wale wanaharusi waliona thamani ya YESU na kumwalika katika sherehe yao, na pale walipopungukiwa ndipo Kristo alipozuchukua fadhaa zao na aibu yao..
Wenye harusi , (wao hawakumwalika Bwana kwasababu walijua divai itaisha ili baadaye wamwite awageuzie maji kuwa Divai).. La! Ile ilitokea tu kama dharura na ndipo Bwana akafanya miujiza.. Wao lengo lao kubwa lilikuwa ni kumwitaji YESU ndani ya harusi yao, na si wamtumie.
Na sisi leo hatupaswi kumfuata BWANA YESU kwasababu tu tunataka uponyaji, au heshima au kuinuliwa kimaisha (watu wote waliomfuata Bwana YESU kwa haja kama hizo aliwakimbia Soma Yohana 6:25-26)..Lakini tumfuate Bwana YESU kwasababu tunataka uzima kwanza, na kuyafanya mapenzi yake na hayo mengine yawe ni dharura tu, kama wale waliomwalika.
Ukishahikiki kwamba uzima upo ndani yako, ndipo tumtwike hayo mengine..
1Petro 5:7 “huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Manabii walisema “Neno la Mungu likanijia” ..Maana ya hili neno ni nini?.
Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.
WENGINE WANAKESHA KWAAJILI YAKO.
BUSTANI YA NEEMA.
MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.
Rudi Nyumbani
Print this post