Swali: Kwanini biblia ikataze kujiongezea hekima, kwani kuna ubaya gani katika kuongeza hekima?
Jibu: Turejee..
Mhubiri 7:16 “Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe?”.
Hekima inayozungumziwa hapo si hekima ya KiMungu, ambayo hiyo tumeagizwa tuitafute sana..
Yakobo 1:5 “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa”.
Tena maandiko yanasema mtu aonaye hekima (hiyo ya kiMungu), biashara yake ni Zaidi ya fedha..
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.
14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye”.
Kwahiyo hekima iliyozungumziwa hapo katika Mhubiri 7:16b ambayo mtu akiwa nayo nyingi inamharibu si hekima ya kiMungu, bali ni HEKIMA YA KIDUNIA.. Ambayo hiyo kwa Mungu ni upuuzi sawasawa na 1Wakorintho 3:18
1Wakorintho 3:18 “Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.
19 Maana HEKIMA YA DUNIA HII NI UPUZI MBELE ZA MUNGU. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.”
Umeona?.. kumbe hekima ya dunia ni upuuzi mbele za Mungu na hiyo mtu akijiongezea sana itamwangamiza!!!.
Sasa mfano wa hekima ya kidunia ni ile inayosema “mwanadamu asili yake ni nyani”.. sasa hii ni elimu/hekima ya kidunia..ambayo imetukuka miongoni mwa wasomi wengi wakubwa, kiasi kwamba mtu aliyezama sana katika hiyo hekima, anajiangamiza mwenyewe, kwani atafikia hatua ya kusema hakuna MUNGU.
Ndio maana hapo biblia inasema “usijiongezee mno”… Maana yake usizame sana katika kuzitafuta, kwani zimejaa upotofu mwingi na ukweli kidogo…
Bwana atusaidie.
Kwa maarifa Zaidi kwanini biblia iseme “usiwe na haki kupita kiasi” fungua hapa >>>>>USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kwanini Mungu alimkataa Sauli? (1Samweli 15:23)
NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?.
Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?
About the author