FUNDISHA NENO KANISANI NA NYUMBANI.

FUNDISHA NENO KANISANI NA NYUMBANI.

(Masomo maalumu kwa wazazi/walezi).

Ni nini unafanya kama mzazi uwapo nyumbani?.. Je maisha yako ndani ya kanisa ni sawa na yale nje ya kanisa?..Je kile unachokifanya kanisani ndicho unachokifanya nyumbani?…je nyumbani kwako ni sehemu ya kuishi tu au ni sehemu pia ya ibada?.

Kama wewe ni mwalimu kanisani, ni lazima pia uwe mwalimu nyumbani kwako…kama wewe ni kiongozi katika nyumba ya Mungu ni lazima pia uwe kiongozi katika nyumba yako, kama wewe ni mchungaji katika nyumba ya Mungu ni lazima pia uwe mchungaji katika nyumba yako mwenyewe…Ndivyo biblia inavyotufundisha.

Mitume wa Bwana YESU ni kielelezo kwetu, wao walikuwa wakihubiri Neno HEKALUNI NA NYUMBANI, kama maandiko yanavyosema, hivyo kama na sisi tumejengwa juu ya msingi wao ni lazima tufanye kama wao walivyofanya..

Matendo 5:42 “Na kila siku, NDANI YA HEKALU na NYUMBANI MWAO, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo”.

Umeona?.. Si hekaluni tu!, bali hata nyumbani…. Uharibifu mkubwa shetani anauanzia nyumbani… Hivyo ni lazima uwe na AMRI, katika nyumba yako mwenyewe… Ni lazima pafanyike ibada nyumbani kila siku, ni lazima pafanyike maombi, ni lazima watoto na wengine wanaoishi katika nyumba yako wajue kuomba na kuombea wengine.

Ni lazima watoto wajifunze biblia na kufundisha biblia tangu wakiwa wadogo, ni lazima pia wajifunze kutoa.. ni lazima wote wawe wa kiroho, ni lazima uwafundishe wawe vipaumbele katika Imani wawapo shuleni, maana yake wakiwa shuleni wawe vipaumbele katika kuongoza maombi kwa wanafunzi wenzao, na kuomba vile vile kufunga… Na si kuwaacha jumapili kwa jumapili  tu wafundishwe kanisani hayo mambo..

Jenga tabia ya kuwafuatilia mienendo yao ya kiimani wakiwa mashuleni, fuatilia sifa zao za kiimani wawapo mashuleni, (na si tu taaluma yao)..wapo watoto taaluma zao zinaonekana nzuri lakini shetani kashawaharibu kitabia muda mrefu (matokeo yake yatakuja kuonekana baadaye).

Hivyo kama mzazi au mlezi, simama katika hiyo nafasi… kiasi kwamba NENO LA MUNGU nyumbani kwako ni AMRI sio OMBI!. Kama Nabii Yoshua alivyoazimia zamani zile..

Yoshua 24:15 “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; LAKINI MIMI NA NYUMBA YANGU TUTAMTUMIKIA BWANA.

16 Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache Bwana, ili kuitumikia miungu mingine”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KUOTA UPO KANISANI.

UWE MWAMINIFU HATA KUFA.

NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?

YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.

Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments