Heshima ni kitendo cha kumpa mtu hadhi yake, au uthamani wake anaostahili. Kwa kawaida kila mwanadamu anastahili heshima. Na hivyo kama mwamini huna budi kujua jinsi ya kuigawanya heshima kulingana na mtu husika. Kwasababu ukosefu wa heshimu, kwanza ni zao la kiburi (Mithali 15:33), lakini pia hukuondolea Baraka na kibali popote pale uendapo. Lakini pia ukitoa heshima isiyompa mtu ni kosa pia.
Warumi 13:7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima
Kutii maelekezo yao.
Waebrania 13:17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
Kutowakwaza,
Waefeso 6:4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
Kutenda agizo lao.
Warumi 13:1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu
Kuwatumikia kwa uaminifu na adabu. (Waefeso 6:5-8)
Hivyo kwa hitimisho, ni kwamba kila mwanadamu anastahili heshima, haijalishi, tajiri, au maskini, mrefu au mfupi, mgonjwa au mzima, mwenye elimu au asiye na elimu, bwana au mtumwa, ameokoka au hajaokoka. Wote ni agizo tuheshimiane.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author