TUNZA MAVAZI YAKO NA FUA NGUO ZAKO!

TUNZA MAVAZI YAKO NA FUA NGUO ZAKO!

Vazi/Nguo kiroho linawakilisha “matendo ya mtu”, maana yake kiroho mtu mwenye mavazi masafi, maana yake matendo yake ni masafi, na kinyume chake mwenye mavazi machafu maana yake matendo yake si safi (Ufunuo 19:18).

Sasa Matendo yanatunzwa, lakini pia yanafuliwa (safishwa).. kama vile nguo inavyoweza kutunzwa lakini pia kufuliwa.

     1. TUNZA MAVAZI YAKO.

Maana ya kutunza mavazi ni kuhakikisha hayaharibiki wala kuwa na kasoro yawapo mwilini. Vazi lililotoboka au kuchanika maana yake limekosa matunzo mwisho wa siku yule mtu atabaki Tupu.

Vivyo hivyo ni wajibu wetu kuyatunza Matendo yetu mema, yasiharibike.. Kwa kujiangalia mazingira tuliyopo na mambo tuyafanyayo…

Ufunuo 16:15” (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, NA KUYATUNZA MAVAZI YAKE, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake)”.

Vitu vinavyoharibu matendo yetu mazuri/tabia nzuri ni pamoja kampani tulizonazo na mazungumzo tuzungumzayo..

1Wakorintho 15:33 “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”.

Chunguza makundi uliyonayo na aina ya mazungumzo unayozungumza.

      2. FUA NGUO ZAKO.

Nguo isiyofuliwa inapoteza umaridadi na unadhifu kwa mtu, hata kama haijaharibika au kuchanika. Vile vile Matendo yasiyofuliwa yanapoteza unadhifu wa mtu kiroho.

Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13  Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

14  HERI WAZIFUAO NGUO ZAO, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”.

Sasa mtu anafuaje Matendo yake?… Si kwa njia nyingine Zaidi ya kuomba na kusoma Neno.

Na Utajuaje matendo yako yameanza kuingia dosari?.. si kwa kusubiri uambiwe na mtu au watu, bali kwa kusoma Neno (biblia). Unaposoma Neno ndipo utakapojijua kama una kasoro au la!, kwasababu Neno la Mungu ni kioo.. Ili ujijue kama una uchafu mwilini, si kusubiri uambiwe, kwasababu si wote wenye ujasiri wa kukwambia kasoro zako.

Kitu pekee kitakachoweza kuutambulisha uchafu usoni mwako ni KIOO

na ni lazima usomaji wa Neno uambatane na maombi.

Hivyo Maombi ni “Maji” na Neno la Mungu ni “sabuni” kwa mambo hayo, matendo yetu yatakuwa safi daima.

Bwana atuongezee Neema yake.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?

MAVAZI YAPASAYO.

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

JE! UNA MHESHIMU MUNGU?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments