Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe. Karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo Mwanga wa njia yetu na Taa iongozayo miguu yetu (Zaburi 119:105).
Wengi tuna juhudi katika “mwili” lakini hatuna juhudi katika “roho”. Juhudi katika mwili ni nzuri na inafaa lakini ile ya roho ni bora Zaidi na inafaa sana. Kwasababu biblia inasema Roho ndiyo inayoutia uzima (Yohana 6:63).
Sasa Neno la Mungu linasema..
Warumi 12:11 “kwa bidii, si walegevu; MKIWA NA JUHUDI KATIKA ROHO ZENU; mkimtumikia Bwana”.
Sasa hizi juhudi katika roho ni zipi?..
1. JUHUDI KATIKA MEMA.
1Petro 3:13 “Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema”.
Matendo mema ni pamoja na kuwasaidia wanyonge (masikini, wayatima na wajane), kusamehe na mengineyo..
2. JUHUDI KATIKA KUPENDANA.
1Petro 4:8 “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
9 Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika”
Mtu mwenye juhudi katika roho ni yule pia mwenye juhudi katika kuutafuta upendo.
3. JUHUDI KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU.
Kazi ya Mungu si lazima iwe ule ya kusimama mimbarini na kuhubiri/kufundisha.. Lakini pia ile ya kusafisha nyumba ya Mungu, ni kazi yenye thawabu kubwa na heshima kubwa kwa Mungu… Ukiwa na juhudi katika kumtumikia Mungu kwa njia hiyo pasipo kusukumwa au kukumbushwa kumbushwa bali unajituma wewe mwenyewe, basi hapo unaonyesha juhudu uliyonayo katika roho, na ukomavu wako kiroho.
4. JUHUDI KATIKA KUOMBA.
Ikiwa utaweza kuomba kila siku kwa muda usiopungua lisaa limoja, hiyo ni ishara kubwa ya kuwa una juhudi katika roho, lakini kama kuomba kwako ni mpaka jumapili kwa jumapili, basi kuna ulegevu ulio ndani yako.
5. JUHUDI KATIKA KUSOMA NENO.
Mtu mwenye kutia bidii katika kujua mafunuo yaliyo ndani ya biblia kwa njia ya kujifunza na kutafiti na kurudia rudia kutafakari yale aliyoyasoma na kujifunza, mtu wa namna hiyo kibiblia ni mwenye juhudi katika roho na si mlegevu.
Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.
6. JUHUDI KATIKA KUMTOLEA MUNGU.
Sadaka inakamilisha ibada kwa mkristo yoyote yule (ikiwemo mchungaji, mwalimu, nabii, mwinjilisti au mtumishi mwingine yoyote). Na mtu mwenye bidii nyingi katika kumtolea Mungu, mtu huyo kulingana na biblia ni mwenye juhudi katika roho.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kwa namna gani mauti ya wacha Mungu ina thamani machoni pake? (Zaburi 116:15).
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.
IKIWA MWENYE HAKI AKIOKOKA KWA SHIDA, MWENYE DHAMBI ATAONEKANA WAPI?
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
Ni kwa namna gani, upendo husitiri wingi wa dhambi? (1Petro 4:8).
About the author