Ni alama gani Mungu aliyomtia Kaini mwilini? (Mwanzo 4:15)

Ni alama gani Mungu aliyomtia Kaini mwilini? (Mwanzo 4:15)

SWALI:Ni alama gani Mungu aliyomtia Kaini mwilini?


Tunaona Kaini baada ya kumuua ndugu yake Habili, Mungu alimpa adhabu kwa kumwambia maneno haya;

Mwanzo 4: 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

Lakini tukiendelea kusoma tunaona, Kaini anamlilia Mungu na kumwambia adhabu yangu ni kali sana, haichukuliki, kila mahali nitakapoenda nitakuwa mtu wa kuuliwa, ndipo Mungu akamuhakikisha ulinzi kwa kumwekea alama. Kama tunavyosoma kwenye vifungu vinavyofuata;

13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.

14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.

15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga

Swali linakuja hii alama ni ipi?

Lakini kabla ya kufahamu alama yenyewe ni nini ni vizuri ukaelewa maana ya adhabu aliyopewa ya kuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. Fungua hapa ufahamu tafsiri yake >>>> UTAKUWA MTORO NA MTU ASIYE NA KIKAO DUNIANI.

Hivyo tukirudi kwenye swali alama ni ipi?

Zipo nadharia nyingi, lakini tujifunze kwanza baadhi ya mambo.  Kumbuka kuwa adhabu ile Kaini aliitambua kabisa ilihusu kutengwa na fadhili na uso wa Mungu kabisa. Na mahali popote pasipo na mkono wa Mungu hapana usalama wowote, ni sawa na mwili unaokosa kinga, kila  ugonjwa unaopita pale utaushambulia, hata yale maradhi madhaifu kabisa,. Ndicho alichokigundua Kaini alijua pasipo Mungu duniani hata kwa sehemu ndogo, haiwezekaniki  kuishi, chochote chenye  uhai atakuweza tu, wanyama watakuweza, mapepo yatakuweza. Ndio maana ya kauli yake hiyo ‘kila anionaye ataniua’.

Lakini Mungu akamuhakikishia usalama, kwa kumwekea alama, ili yoyote akimwona asimuue Kaini. Sasa kufikiri alama hiyo ni mchoro(tattoo) Fulani mwilini, si rahisi kumfanya mtu asidiriki kumuua, kwani mchoro hauzuii mtu kuangamizwa.

Lakini kufikiria alama iliwekwa katika eneo la ki-mwonekano (ukubwa), au eneo la kuongezewa sifa/ufanisi Fulani uliotofauti na wengine yaweza kuwa jambo la kweli.

Kwanini?

Tunaweza kuona baada ya pale sifa za uzao wa Kaini jinsi zilivyokuwa, walikuwa ni watu wavumbuzi, watu wa elimu (Mwanzo 4:20-22) lakini pia Hodari na wengine wao wenye maumbo makubwa (Mwanzo 6:4),.  Kwahiyo sikuzote tunafahamu hata sasa walio na uwezo mkubwa wa kielimu na kiteknolojia si rahisi kuwaweza kivita, hata iweje. Tofauti na uzao wa Adamu kwa Sethi, walikuwa ni wakulima tu na wafugaji. Hawakuwa na ujuzi mwingi ijapokuwa walikuwa ni uzao wa Mungu.

Kwahiyo wana wa Kaini, waliitawala dunia, hawakuwa watu dhaifu dhaifu, na yoyote ambaye angejaribu kumuua mmojawapo, kisasi kingemrudia mara saba, kwa nguvu tu walizokuwa nazo, ijapokuwa hawakuwa na Mungu maishani mwao.

Ni kutufundisha nini?

Si jambo la ajabu Mungu kumuhakikisha ulinzi mtu mwovu, leo hii wengi watasema Bwana mbona wenye dhambi ndio wanaofanikiwa, mbona waovu ndio wenye nguvu duniani, wapo salama, ndio wenye mavumbuzi makubwa. Fahamu kuwa hiyo ni alama yao. Ambayo ilianzia tokea mbali kwa Kaini. Kwasababu wangekuwa waovu, halafu pia wanyonge, wangeishije kwenye hii dunia.

Kamwe usiitamani alama ya Kaini, usitamani kulindwa ndani ya uovu, kwasababu utadumu kwa kitambo tu, baadaye utaangamizwa kama ilivyokuwa kwa hawa, katika gharika. Yesu alitoa mfano wa magugu na ngano katika shamba, kama tunavyoifahamu ile habari, wale wakulima walitaka kwenda kuyang’oa magugu shambani ili waziache ngano. Lakini mwenye shamba akasema waache vyote vikue pamoja mpaka siku ya mavuno, ndipo yatakusanywa na kutupwa motoni.

Na tafsiri ya mfano ya ule mfano akasema shamba ni ulimwengu, na ngano ni wana wa ufalme, lakini magugu ni wana wa ibilisi, na wavunaji ni malaika. Kuonyesha duniani yapo mapando ya aina mbili, na yote yatashiriki mbolea, maji, matunzo yote kutoka kwa Mungu, na kimsingi magugu huwa ndio mepesi kustawi kwa haraka kuliko ngano.

Jiulize na wewe ambaye unastarehe katika dhambi na hauoni madhara yoyote, unaelekea wapi? Hujui umetiwa alama kwa muda, nguvu zako, utajiri wako, mafanikio yako, zaidi ya watu wa Mungu, usidhani ndio umebarikiwa unathamini na Mungu.  lakini wakati utafika kuzimu utaiona.  Embu kubali sasa kuwa mwana wa ufalme, kwa kumaanisha kutubu dhambi, na kumfanya Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, ili akuondolee deni la dhambi uwe mtakatifu mbele zake kwa damu yake, akuepushe na hukumu inayokuja .

Ikiwa upo tayari kuokoka leo. Fungua hapa >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

Nitamjuaje nabii wa Uongo?

USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments