TUNAPASWA TUWEJE WAKATI WA KUJA KWAKE  BWANA YESU?.

TUNAPASWA TUWEJE WAKATI WA KUJA KWAKE  BWANA YESU?.

Ipo hali ambayo tunapaswa tukutwe nayo wakati wa kuja kwake Bwana YESU…na endapo akitukuta tupo nje na hiyo hali basi hatutaenda naye, badala yake tutabaki na kukumbana na hukumu ya MUNGU.

Sasa “hali” hiyo ni ipi?..

Hebu tusome maandiko yafuatayo.

1 Wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, WAKATI WA KUJA KWAKE BWANA WETU YESU KRISTO”.

Kumbe Bwana YESU atarudi tena!!!!….. na wakati atakaporudi anatazamia  tuwe tumetakasika katika maeneo hayo matatu 1) NAFSI 2) ROHO na 3)MWILI.

Vinginevyo mambo hayo matatu yasipokuwa masafi wakati wa kuja kwake Bwana YESU basi kuna hatari kubwa sana.

1.NAFSI.

Ndani ya nafsi kuna maamuzi, hisia na mawazo.. Hivi vinapaswa viwe visafi daima.

Na vinakuwaje visafi?… Kwa kumpokea YESU, kusoma Neno na kuomba.

Usipokuwa mwombaji nafsi yako haiwezi kuwa safi utakuwa mtu wa hasira tu, mtu wa uchungu tu..usipokuwa msomaji wa Neno la Mungu kamwe nafsi yako haiwezi kustahimili majaribu na pia utakuwa mtu usiye na mwongozo n.k.

2.ROHO.

Ndani ya roho ya mtu kuna uzima, na ndio chumba pekee cha ibada ambacho kinaongozwa na Imani. 

Roho ya mtu isipokuwa safi, mtu huyo hawezi kwenda na Bwana siku ya unyakuo…na hata maisha yake ya duniani hawezi kumwona Mungu.

3. MWILI.

Mwili ni vazi la roho ya mtu, na ndilo limejumuisha viungo vyote vya ndani na nje.

Na mwili unapaswa uwe safi (usafi wa kimatendo)..Mwili mchafu kibiblia sio ule wenye jasho au vumbi…mwili mchafu ni ule unaofanya uasherati na zinaa, ni ule unaojichua, ni ule unaotembezwa uchi barabarani, ni ule unaoshika fedha za wizi na utapeli.

Huo ndio mwili mchafu, ambao kama hautatakaswa wakati wa kuja kwake Bwana utampoteza mtu huyo.

Na mtu hautakasi mwili wake kwa kuoga na maji moto, au kwa kumeza vidonge vya matibabu au mitishamba…bali kwa kuacha matendo yote ya mwili yanayotajwa katika Wagalatia 5:19-20.

Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 

20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 

21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.

Kwa hitimisho ni kwamba kila mtu lazima ajitakase na kuhifadhi utakaso wake ambao ndio tiketi ya kumwona Bwana siku atakaporudi.

1 Wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, WAKATI WA KUJA KWAKE BWANA WETU YESU KRISTO”.

Je umempokea Bwana YESU?…Kama bado unasubiri nini??… Na kama tayari umeshampokea je! umetakaswa nafso yako, roho yako na mwili wako?..

Kwa mwongozo wa maombi ya kujijenga kiroho juu ya mambo hayo matatu (nafsi, mwili na roho) basi wasiliana nasi inbox.

Maran atha!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MCHE MWORORO.

KWANINI TUNAPASWA KWENDA KUIHUBIRI INJILI KWA UJASIRI WOTE?

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

JITAHIDI KUJA KABLA YA WAKATI WA BARIDI.

Biblia inamaanisha nini kusema Yeye aliye na sikio, na asikie?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments