Kwanini matajiri wanaambiwa walie na kupiga yowe (Yakobo 5:1-6)

Kwanini matajiri wanaambiwa walie na kupiga yowe (Yakobo 5:1-6)

Yakobo 5:1-6

Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia.

Biblia inatoa angalizo na tahadhari katika eneo la watu wanaoitwa matajiri. Kimsingi utajiri si dhambi, na ni mapenzi ya Mungu watu wake wafanikiwe, (lakini si katika hila).

Hivyo biblia inafunua siri za matajiri wengi wadhalimu, na kuwaonya mapema ili wajirekebishe kwasababu kuna adhabu kali wameandaliwa mbeleni kwa ajili yao.

Biblia inafunua vyanzo vikuu vya mafanikio yao, wala sio katika uchawi kama wengi wanavyodhani,.. bali vipo kwa “wale watu wawatumikiao”, walio chini yao, au wanaowatumia kufanya shughuli zao.

Matajiri wengi, huwatumia wao kama daraja la wao kufika juu, ndio hapo hutumia njia ya kuwatumikisha zaidi ya kawaida yao, na kuwalipa mishahara midogo, au hata wakati mwingine kuwadhulumu kabisa kutowapa kitu, na kuwanyanyasa, hawajali malalamiko yao, na changamoto zao na mahitaji yao. Wanachojali ni kiasi gani kimepatikana, au kazi ngapi zimekamilika. Ili wapate fedha wakazijaze hazina zao.

Lakini Hawajui kuwa Kilio chao kinamfikia Mungu mbinguni. Ijapokuwa wao wanaweza wasione chochote. Kumbe hawajui wanajikusanyia adhabu kali siku ile ya hukumu.

Biblia imetumia mfano wa “bwana na mkulima wake” aliyemwajiri kwenye shamba lake… akiwawakilisha watu wote wenye wafanya-kazi chini yao.

Anasema..

Yakobo 5:1-6

[1]Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia.

[2]Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo.

[3]Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho.

[4]Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.

[5]Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.

[6]Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.

Umeona? wamejilisha mioyo yao utajiri, wamejinenepesha tayari kwa machinjo yao wenyewe..

Hiyo ndio sababu pale mwanzo anatangulia kwa kusema “walie, na kupiga yowe”, kwa hiyo adhabu kali inayokuja juu yao…yaani akimaanisha watubu haraka sana, ili mabaya hayo yasiwakute.

Ujumbe huu ni hata sasa?

Yaweza kuwa bado hujafikia kiwango cha utajiri wowote lakini hata ukiwa na mtu/watu uliowaajiri chini yako, bado upo kwenye mkondo huo huo wa matajiri,

hivyo wajali sana watumwa wako wape maslahi yao,.sikiliza sana malalamiko yao, kuwa tajiri usiye na lawama, mfano wa Ayubu, ambaye aliwathamini sana watumishi wake mpaka akasema..

Ayubu 31:13-15

[13]Kama nimeidharau daawa(mashtaka) ya mtumishi wangu, au ya kijakazi changu, Waliposhindana nami;

[14]Basi Mungu atakapoinuka nitafanya nini? Naye atakapozuru, nitamjibuje?

[15]Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?

Kuwa tajiri kwa kutenda mema, hapo ndipo baraka zitakapokuja.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.

Mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?

Elewa maana ya Mithali 18:23 Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali. 

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments