Maana ya Mithali 10:1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;

Maana ya Mithali 10:1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;

SWALI: Naomba kuelewa tafsiri halisi ya maneno tuyasomayo kwenye Mithali 10:1.

Mithali 10:1

[1]Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.


JIBU: Mpumbavu kibiblia ni mtu yeyote aliyemkosa Mungu ndani yake, ambaye kwa njia hiyo anaweza kuonyesha tabia yoyote mbaya, aidha wizi, au kiburi, au umalaya, au uchawi, au hasira, mwingine atakuwa mlevi, mtukanaji, mwongo, jambazi, mchoyo, mbinafsi, mkorofi n.k.

Chimbuko ni kumkosa Mungu ndani yako.

Sasa mwana wa namna hii kibiblia sio tu anaiathiri roho yake lakini pia hata waliomzaa.

Mithali 10:1

[1]Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.

Lakini kauli hiyo inapaswa eleweke vizuri, sio kwamba mwana akiwa na hekima ni furaha ‘tu’ kwa baba, mama hausiki, au akiwa mpumbavu ni mzigo tu kwa mama baba hausiki.

Hapana, mambo hayo yanawapata wote.. akiwa na hekima wote hufurahi, vilevile akiwa mpumbavu wote huhuzunika.. Ndio maana sehemu nyingine anasema..

Mithali 17:25

[25]Mwana mpumbavu ni huzuni kwa babaye, Na uchungu kwa mamaye aliyemzaa.

Wazazi wote hufurahishwa au huhuzunishwa kwa tabia husika za watoto wao.

Lakini alipoonyesha kama kuwatenganisha, ni kuelezea ‘hisia za juu zaidi’ zitokeazo kulingana na mzazi na mzazi.

Kimsingi mtoto akiwa na hekima, baba huwa anajivunia sana mtoto huyo, utaona baba anajigamba kwa ajili ya mwanae..Mfano tu wa Sulemani kwa Daudi, hekima yake ilikuwa ni fahari ya babaye Daudi.

Lakini akiwa ni mpumbavu, tengeneza picha mtoto ni teja, na kibaka, na mlevi, kiuhalisia utaona akina mama ndio wanateseka zaidi na kuumia juu ya watoto wao. Wanapatwa na mzigo mzito sana moyoni. Na hiyo huwa inawasukuma kuzunguka huku na huko kutafuta msaada. Tofauti na wababa, watamwonya, mara ya kwanza, mara ya pili, mara ya tatu wakiona haonyeshi geuko lolote, ni rahisi kuachana nao.

Ni nini tunaonyeshwa rohoni?

Si mwilini tu. Rohoni Kristo anafananishwa na Baba, na Kanisa lake ni Mama.

Wote sisi ni watoto ambao Kristo ametuzaa ndani ya kanisa lake, tuwapo na hekima (tunamcha), tunatembea katika misingi ya Neno lake, kwa kuzingatia viwango vya upendo na utakatifu, tujue kuwa Kristo hutukuzwa na hujivunia sana sisi. Lakini tuwapo wapumbavu, tunajiumiza zaidi sisi wenyewe. Kwamfano sababu mojawapo ipelekeayo makanisa kupoteza furaha na amani,  ni kukosekana umoja na upendo.

Bwana atusaidie.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.

MJUE SANA YESU KRISTO.

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments