Swali: Ni kwanini siku/saa ya kuja kwa Bwana YESU anaijua Baba peke yake na mwana haijui?, na ilihali pia YESU ni Mungu?
Jibu: Turejee..
Mathayo 24:36 “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
Kipindi Bwana YESU yupo duniani, alikuwa hana budi kuwa kama wanadamu wengine, ingawa alikuwa na uungu ndani yake, Hivyo alikuwa anahisi maumivu kama watu wengine,… alikuwa anasikia huzuni kama tu watu wengine, na pia ilimpasa amtafute Mungu kama tu wanadamu wengine wanavyomtafuta, ndio maana alifunga na kukesha milimani kuomba kwa machozi, ili aweze kupokea mafunuo kutoka kwa Baba, kwaajili ya huduma yake na watu wake.
Waebrania 5:7 “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu.
Hivyo Bwana YESU hakuzaliwa anajua vyote, ilimpasa ajifunze vitu.. alizaliwa hajui kutembea na hivyo ikampasa ajifunze kutembea kama watoto wengine, vile vile alizaliwa hajui kusoma na hivyo ilimpasa ajifunze kusoma na pia ajifunze torati.
Luka 2:46 “na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta.
46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.”
Hivyo kwa tabia hiyo ya kuendelea kujifunza, ni wazi kuwa si vyote alikuwa anavijua kipindi yupo duniani, ndio maana akasema “ile siku hata yeye haijui”
Lakini alipokufa na kufufuka, mambo yakageuka… ALIJUA YOTE!!, kwani baada ya kufufuka alisema, amepewa mamlaka yote ya mbinguni na duniani.
Mathayo 28:16 “Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.
17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”.
Sasa hawezi kupewa mamlaka yote mbinguni, halafu asijue saa ya kuja kwake, ni jambo lisilowezekana…
Kiashiria kingine kinachoonesha kuwa Bwana YESU aliijua saa ya kurudi kwake, baada ya kufufuka ni lile neno alilomwambia Petro kumhusu Yohana kwamba “ikiwa anataka akae hata ajapo” soma Yohana 21:22.
Soma pia Ufunuo 3:3, Ufunuo 16:15, Ufunuo 22:12, na Ufunuo 22:20.. Utaona mamlaka ya YESU kuhusiana na kurudi kwake.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Bwana YESU KRISTO sasahivi anajua kila kitu, ikiwemo siku ya kurudi kwake mara ya pili, na mwisho wa dunia (Si wa kawaida kabisa!!)
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
TUNAPASWA TUWEJE WAKATI WA KUJA KWAKE BWANA YESU?.
Maana ya Mhubiri 10:15 Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja,
About the author