Swali: Je malaika wana damu na nyama na mifupa kama tuliyonayo sisi wanadamu?
Jibu: Malaika wanayo miili kama wanadamu tulivyo na miili, isipokuwa miili ya Malaika imeumbwa kwa malighafi za kimbinguni na hii yetu imeumbwa kwa udongo.
Na kwasababu miili ya Malaika imeumbwa kwa malighafi ya kimbinguni, basi uwezo wake au fahari yake ni kubwa kuliko hii yetu ya udongo, yenyewe haimwi, haichoki, haina tamaa, wala haifi…
1Wakorintho 15:40 “Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali”.
Miili ya Malaika inaweza kubadilika na kuwa ya kibinadamu kwa muda, na kwa kusudi maalumu, ndio maana katika biblia tunaona Malaika wakiwatokea watu kama wanadamu (Soma Mwanzo 18:1-3, Mwanzo 32:24, na Yoshua 5:14)… Lakini hii ya udongo haiwezi kubadilika na kuwa ya viumbe wengine, mabadiliko ya miili ya udongo ni unene, wembamba na urefu basi, hivyo ni dhaifu sana..
Lakini pamoja na hayo yote, wanadamu tuliomwamini Bwana YESU na kumfuata tunayo ahadi ya kubadilishwa hii miili na kupewa kama ile ya Malaika watakatifu isiyo na kasoro, (miili ya kimbinguni).. na ahadi hiyo itatimia katika ile siku ya ufufuo kulingana na maandiko..
1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa”
Soma pia Mathayo 22:30..
Sasa tukirudi kwenye swali! Je Malaika wana damu na nyama kama sisi wanadamu?, jibu tumeshapata kuwa HAPANA!, Kwasababu miili yao si ya duniani, inayohitaji oksijeni ili iishi, hivyo hawana damu na nyama.
Je umempokea BWANA YESU?.. Je unaishi katika ahadi hiyo ya kubadilishwa mwili katika siku ile?.. Kama upo nje ya KRISTO, na ikitokea umekufa, basi hutakuwa miongoni mwa watatakaofufuliwa na kuvikwa miili ya kimbinguni.
Bwana atusaidie tusiikose ile ahadi.
Ubarikiwe.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nini Maana ya Adamu?
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
WEWE SI MALI YAKO MWENYEWE!
About the author