Je! Yusufu aliwezaji kutafsiri ndoto?

Je! Yusufu aliwezaji kutafsiri ndoto?

SWALI: Yusufu aliwezaji kutafsiri ndoto? Je ni kwa hekima aliyokuwa nayo au kwa kuangalia ishara fulani, au kwa usomaji wa vitabu, au kwa saikolojia?


JIBU: Biblia inatuonyesha sifa kuu, ya Yusufu iliyokuwa ndani yake ni uwezo wa kutafsiri ndoto.

Lakini swali linaloulizwa je uwezo huo alitolea wapi, ulikuwa ndani yake mwenyewe au ulitoka kwingine.

Tukisoma  Mwanzo 41:15, tunaweza kupata majibu;

Farao akamwambia Yusufu, Nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri.16 Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani.

Hapo Yusufu anasema si mimi, Mungu atampa Farao majibu. Kuonyesha kuwa uwezo huo ulitoka kwa Mungu wala sio katika akili zake, elimu , saikolojia , au hekima ya kibinadamu.

Alimtegemea Mungu asilimia mia kumfunulia, mfano tu wa Danieli alipokwenda kuomba juu ya tafsiri ya ndoto ya Nebukadreza katika sala akafunuliwa. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yusufu, katika kutafsiri ya ndoto ya Farao, pamoja na za wale watumishi wawili wa mfalme waliokuwa wanahudumu mezani pa mfalme. Hakubuni tu tafsiri kulingana na mazingira, bali alifunuliwa moja kwa moja aidha kwa ndoto au kuona maono.

Lakini ni kwanini Yusufu apokee neema hiyo kirahisi kwa Mungu, tofauti na wengine.

Jibu lipo katika TABIA yake, Ni wazi Roho ya Mungu huvutika sana katika tabia njema ya mtu. Yusufu tangu udogo alijitahidi kujiepusha na tabia zisizofaa, jambo lililopelekea mpaka ndugu zake kumchukia kwasababu alikuwa anatoa siri za mambo yao mabaya, hata alipouzwa kwa akida wa Farao, bado aliendeleza tabia yake ileile, pale mke wa Potifa alipomtamani akakataa, mwishowe akatupwa gerezani. Kwa njia hiyo Yusufu hakuacha kulitunza joto la ROHO ndani yake. Mfano tu wa Danieli naye, ambaye hakutaka kujitia unajisi kwa vyakula vya kifalme, na ndani ya hakukuonekana kosa lolote (Danieli 6:3).

Akashuhudiwa na mfalme kuwa  Roho njema sana, na iliyo bora inakaa ndani yake.

Danieli 5:12 kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danielii, naye ataionyesha tafsiri.

Hivyo ili na sisi tushiriki sehemu bora na njema za vipawa mbalimbali vya Roho Mtakatifu, hatuna budi kujijenga  kimwenendo, katika maisha matakatifu yampendezayo Mungu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?

KWA KUWA ROHO BORA ILIKUWA NDANI YAKE.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments