Kuonja ni kufanya nini? (Kutoka 15:25).

Kuonja ni kufanya nini? (Kutoka 15:25).

Swali: Kuonja kunakozungumziwa katika kitabu cha Kutoka 15:25 kunamaanisha nini?.

Jibu: Turejee mistari hiyo..

Kutoka 15:24 “Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema,Tunywe nini? 

25 Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, AKAWAONJA HUKO

Kuonja kunakozungumziwa hapo ni kuonja kiroho na si kimwili, siku zote mtu anayeonja kitu, lengo lake ni kukipima ubora wake, kilingana na vigezo anavyovitaka.

Na kiroho MUNGU anatuonja sisi mara kwa mara kwa kuangalia matendo yetu kama tupo sawa mbele zake…

Kwamfano utaona Bwana YESU anatumia lugha hiyo ya kiroho katika kitabu cha Ufunuo kuyapima matendo yetu..

Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”

Umeona hapa?…matendo yetu yanapimwa kwa kinywa cha Bwana..kama tu Moto mbele zake basi tuna heri, lakini kama tu baridi au vuguvugu ni Ole!.

Kwahiyo hata kipindi wana wa Israeli wakiwa wanatoka Misri kuelekea nchi ya ahadi.. Mungu alikuwa anawaonja matendo yao…

Na kuna kipindi aliwatapika walipomjaribu na kumnun’unikia.

Lakini si tu Bwana akiyekuwa anawaonja, bali pia aliwaambia kuwa hiyo nchi wanayoiendea itawaonja matendo yao, na kama yakiwa mabaya itawatapika, kwa kuwa pia iliwatapika wenyeji waliokuwa wanaiishi kutokana na mateendo yao maovu.

Walawi 18:25 “na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi YATAPIKA wenyeji wake na kuwatoa. 

26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 

27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 

28 ili kwamba hiyo nchi ISIWATAPIKE NA NINYI PIA, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu”.

Je umempokea YESU?.

Je wewe ni moto?, au baridi au una uvuguvugu?…Uvuguvugu maana yake ni kuwa upo mguu mmoja nje!…mguu mmoja ndani!, leo unaenda kanisani kesho unaenda Bar, leo unatoa sadaka kesho unabeti, leo unavaa nguo ya sitara kesho nguo ya aibu..hapo Bwana amesema atatapika mtu wa namna hiyo.

Bwana atusaidie tumtii ili tusiwe miongoni mwa watakaotapikwa.

Maran atha!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments