Jibu: Turejee maandiko machache..
“Uhai” ni hali ya kuwa “HAI” (yaani kuishi) ili kiumbe kiwe kinaishi ni lazima kipumue, kile, kikue na hata kijongee. Hizo ndizo tabia chache za viumbe HAI, Wanadamu, wanyama na mimea vyote vina uhai kwasababu vinapumua, vinaongezeka na pia kujongea.
Lakini “UZIMA” Umeenda mbali zaidi kuelezea UHAI wa kiroho ambao unapatikana kwa mtu kuwa na mahusiano na MUNGU.
Uhai unaelezea mwili lakini Uzima unaelezea roho. Mimea haina UZIMA bali ina UHAI.. wanyama hawana UZIMA bali wana UHAI maandiko yanaonyesha hivyo…
Mithali 12:10 “Mwenye haki huufikiri UHAI WA MNYAMA WAKE; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili”.
Na UZIMA unapatikana kwa mmoja tu ambaye ni YESU KRISTO,
Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili WAWE NA UZIMA, kisha wawe nao tele”.
ikiwa na maana kuwa wanadamu yoyote aliye nje ya YESU KRISTO anao “Uhai” tu kama wanyama lakini hawana “Uzima”… anapumua, anakula, anatembea lakini akisha kufa hana UZIMA tena.. Lakini aliye ndani ya KRISTO, hata akiwa amekufa ataendelea kwasababu anao UZIMA wa MILELE alioupokea kutoka kwa YESU.
Je unao uzima wa milele ndani yako?…Je YESU ni sehemu ya maisha yako?
Yohana 17:2 “kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape UZIMA WA MILELE.
3 Na UZIMA WA MILELE ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na YESU KRISTO ULIYEMTUMA”.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JE! UPO KATIKA MAJI YA UTULIVU?
Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?
Kwanini pawekwe MITI pale bustanini na si kitu kingine?.
About the author