Nini maana ya “mtu atachukua dhambi zake” (Walawi 5:17).

Nini maana ya “mtu atachukua dhambi zake” (Walawi 5:17).

Swali: Neno la MUNGU linamaanisha nini linaposema “mtu atachukua dhambi yake au uovu wake”?

Jibu: Turejee andiko hilo..

Walawi 5:17 “Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia vivyo, NAYE ATACHUKUA UOVU WAKE”

Tusome tena..

Walawi 24:5 “Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu awaye yote atakayemlaani Mungu wake ATACHUKUA DHAMBI YAKE”.

Utalisoma tena neno kama hilo katika Walawi 7:18, Hesabu 9:13, Ezekieli 44:10-12..

Katika  Agano la kale Bwana MUNGU aliruhusu mtu kulipizwa kisasi endapo amefanya jambo la kusudi lililo baya.. kwamba UHAI kwa UHAI.. jino kwa jino..jicho kwa jicho..

Maana yake kama mtu amemkata mwenzake mkono naye pia ni lazima akatwe mkono, kama mtu amemwua mwenzake sharti naye pia auawe..

Walawi 24:17 “Na mtu ampigaye mtu hata akafa, lazima atauawa;

18 na atakayempiga mnyama hata akafa atalipa; uhai kwa uhai.

19 Na mtu akimtia mwenziwe kilema; vile vile kama alivyofanya, naye atafanyiwa vivyo;

20 jeraha kwa jeraha, jicho kwa jicho, jino kwa jino; vile vile kama alivyomtia mtu kilema, naye atalipwa vivyo”.

Lakini yapo matukio ambayo yalikuwa yakifanyika yanakuwa HAYANA KISASI!, kwamfano mtu aliyesikika kamtukana MUNGU au kulilaani jina la MUNGU, mtu huyo sheria ilikuwa ni kuuawa kwa kupigwa mawe, sasa wale watu waliomwua kwa kumpiga mawe baada ya kuthibitika uasi wa Yule mtu, hao hawawezi kulipwa kisasi kwamba nao wauawe kwasababu sheria imesema uhai kwa uhai.

La! Bali wataachwa hai,.. sasa hiko kitendo cha hawa wauaji kuachwa Hai na kutokulipwa kisasi ndio tafsiri yake kwamba “Yule aliyekufa kauchukua uovu/dhambi yake mwenyewe”.. maana yake hajaacha dhambi kwa waliomwua!.

Lakini laiti kama atauawa pasipo hatia na ikathibitika hivyo, basi wauaji wale watabeba dhambi ya mauaji hivyo nao pia watauawa, kama sheria isemavyo kwamba uhai kwa uhai na jino kwa jino. Sasa kitendo hiko cha kuuawa kwa kosa la mauaji yasiyo na hatia, ndicho kinachoitwa kubeba dhambi ya aliyekufa.

(kumbuka si kwamba watabeba makosa ya Yule mtu, la!, Yule mtu atabaki na dhambi zake alizozifanya.. bali hawa wauaji watabeba lile kosa moja tu la mauaji ya mtu asiye na hatia), hivyo watahukumiwa tu kama wauaji waliomwua mtu asiye na hatia.

Na lugha nyingine ya kubeba dhambi ya mtu ni kubeba damu ya mtu. Hivyo mahali popote katika biblia Bwana MUNGU anaposema kuwa “nitaitaka damu mikononi mwa mtu” maana yake ni hiyohiyo kwamba “kwamba atamhukumu muuaji kwa kosa la kumwua asiye na hatia”.. na anaposema damu yake itakuwa juu yake mwenyewe aliyefanya kosa, maana yake ni kwamba aliyeuawa hatalipiwa kisasi kwa waliomwua.

Zifuatazo ni baadhi ya dhambi ambazo mtu akizitenda basi alibeba dhambi zake mwenyewe, wala waliomwua hawakuwa na hatia ya kulipwa kisasi wala kushtakiwa.

  1. Kulikufuru jina la MUNGU (Soma Walawi 24:5).
  2. Ibada za sanamu/miungu (soma Kumbukumbu 13:6-12).
  3. Kutoishika pasaka (Hesabu 9:13).
  4. Kufumaniwa katika uzinzi.
  5. Kulala na mnyama wa aina yoyote au ndugu yoyote wa karibu.(Kutoka 22:19)
  6. Kumlaani mzazi (Kutoka 20:9)

Je hata sasa (Agano jipya) sheria hizi zipo?.

Katika Agano jipya hatuna sheria yoyote ya kisasi, Bwana YESU alitufundisha hilo katika Mathayo 5:38-41, ikiwa na maana kuwa hatujapewa ruhusa ya kumwua mtu au kulipiza kisasi bali kisasi ni juu ya Bwana (soma Warumi 12:19).

Kwahiyo kama hatujapewa ruhusa ya kulipa kisasi, au kutoa hukumu ya aina yoyote  kama katika kipindi cha agano la kwanza, basi maana yake ni kwamba mtu yoyote Yule alipaye kisasi atakuwa na hatia pasipo kujalisha makosa aliyoyafanya ndugu yake!..

Muuaji wa aina yoyote ile, atabeba kosa la mauaji, (Bwana ataitaka damu ya aliyemwua mikononi mwake).. hata kama amemwua mtu aliyemlaani MUNGU, bado ni kosa!..katika agano la kale haikuwa makosa lakini agano jipya ni kosa!.

Kwahiyo hatujapewa ruhusa ya kuua kwa kosa lolote lile, tukifanya hivyo tutakuwa na hatia na Bwana ataitaka damu ya aliyekufa mikononi mwetu.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Orodha ya majina ya Miji ya Biblia (Agano la kale) na Sasa

Agano la Chumvi ni nini? (2Nyakati 13:5)

VUNJA AGANO LA MAUTI.

Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?

Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments