Wakamchukua vile vile alivyo katika chombo.

Wakamchukua vile vile alivyo katika chombo.

Marko 4:35-36

[35]Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo.

[36]Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.

Vifungu hivi vinazidi kutueleza tabia ya Bwana wetu Yesu Kristo na huduma yake jinsi ilivyokuwa ya kitofauti sana hapa dunia.

Kujitoa kwake kulikuwa ni kwa gharama sana tofauti na sisi tunavyoweza kufikiri, embu fikiria kisa kile cha pale kisimani alipokutana na yule mwanamke msamaria, na kuanza kumshuhudia habari zake mpaka kupelekea wimbi kubwa la watu Samaria kumfuata.

Kwa jicho la kawaida unaweza kudhani ilikuwa ni huduma ya kawaida lakini kiuhalisia haikuwa ni jambo lililomruhusu sana kimwili. Kwani maandiko yanatuambia alichoka sana kwasababu alikuwa katika safari ndefu kutoka uyahudi Kwenye Galilaya.

Tunasoma akiwa na njaa na kuchoka ‘alijibwaga’ hivyo hivyo pale kisimani, akawaruhusu wanafunzi wake kwenda mjini kutafuta chakula..

Lakini Mwanamke yule alipokuja kisimani hakusema ngoja nipumzike kwanza, nivute pumzi, kinyume chake alianza muda ule ule kusema naye..hata baadaye alipoletewa chakula ale hamu yake ya kula ilikatwa na ile kazi ya Mungu Aliyokuwa anaifanya.

Yohana 4:6-8,30-33

[6]Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.

[7]Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.

[8]Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula…..

[30]Basi wakatoka mjini, wakamwendea.

[31]Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule.

[32]Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi.

[33]Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?

Vivyo Hivyo tena wakati mwingine alikuwa anawahubiria Makutano mchana kutwa, mpaka ilipofika jioni ambapo alipaswa aende kupumzika kidogo, ili kesho aendelee na huduma. Maandiko yanatuambia akawaambia wanafunzi wake “Tuvuke Ng’ambo”.

Kibinadamu jambo kama hilo la safari Nyingine mpya lingetemea kwanza maandalizi fulani labda ya chakula, au mavazi, au kushughulikia mahitaji mengine…lakini kwakua kusudi la Mungu lilimsukuma kwa nguvu wakamchukua Vilevile alivyo katika chombo Mpaka ng’ambo..hakuna kuoga, wala kupumzika, wala kuwatembelea marafiki na ndugu, ni kuunganisha ziara nyingine, sio kwamba alikuwa hachoki hapana alichoka sana, kuthibitisha hilo utaona akiwa katikati Ya safari ile alipitiwa na usingizi kwa sababu ya uchovu (4:38)

Hii inatuonyesha wazi utayari wa Kristo ambao uliathiri mpaka hali zake za kimwili.

Ni kutufundisha nini?

Kwasababu yeye ni yule yule jana na leo na hata Milele, utayari ule ule aliokuwa nao zamani anao hata leo.

Kristo haitaji maandalizi wala hali ya kimazingira, katika kutumika Na sisi. Ni rahisi Kudhani mpaka Bwana atende miujiza tunahitaji kwanza maandalizi ya Maombi na mifungo na mikesha, au mpaka Bwana amwokoe mtu tunahitaji tuwe na elimu nyingi ya biblia, au uzoefu kumbe si lazima..

Ni kweli mambo hayo ni muhimu katika baadhi ya mazingira lakini si yote. Anataka tuwe wepesi wa kumchukua yeye vilevile kama alivyo katika mazingira yoyote?

Yupo tayari kwenda na sisi popote, maadamu tu sisi tunakuwa tayari kumchukua katika safari zetu kwa imani. Hatupaswi kujali tutatolea Wapi fedha za huduma kumuhubiri Kristo.

Ikiwa umeokoka, ni nini unasubiri Usimtumikie Mungu wako?. Unataka uwe kama Martha ambaye alijisumbua na maandalizi mengi wakati lililohitajika ni moja tu, kumsikiliza Kristo? Kumchukua vilevile kama alivyo.

Yesu alipowaacha mitume hakuwapa mitaji ya maspika, au vyuo vya kusoma au majengo ya kuabudia…aliwaambia enendeni nami nitakuwa pamoja nanyi mpaka ukamilifu wa dahari. Msibebe fimbo wala mkoba, wala pesa kibindoni, wala kanzu mbili.(Mathayo 10:5-10)

Kwa tafsiri nyingine anasema nichukueni hivi hivi nilivyo, msijali hali yangu, nanyi mtaona Maajabu mbeleni.

Bwana atujalie kujua matamanio yake, ili tusizuiliwe kuhudumu naye popote, kwenye mazingira yoyote.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Masomo mengine:

RABI, UNAKAA WAPI?

Yesu alipopanda kuomba kwanini atokewe na Musa na Eliya na sio manabii wengine?

SAUTI NYUMA YA ISHARA.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments