Je tamaa ni dhambi kulingana na Yakobo 1:15?

Je tamaa ni dhambi kulingana na Yakobo 1:15?

Swali: “Halafu ile tama ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti, (Yakobo 1:15).. je kutamani sio dhambi?”


Jibu: Kwa asili kutamani sio dhambi! Bali kunaweza kuwa ni mwanzo wa dhambi.. ni sawa na “kuongea”..kuongea si dhambi lakini kunaweza kuwa chanzo cha dhambi, kutegemea ni nini unaongea..

Na vile vile “tamaa” kwaasili ..imeumbwa ndani ya Mtu, na hata ndani ya viumbe vyote, ambayo lengo lake ni kuhamasisha jambo fulani jema au baya lifanyike katika mwili wa mtu au maisha ya mtu.

Kwamfano hatuwezi kumtafuta MUNGU kama yeye mwenyewe hajaiweka hiyo tamaa ndani yetu..hatuwezi kuomba kama yeye hatatuwekea hiyo tamaa ndani yetu n.k

Vile vile katika masuala ya mwilini,  tusingependa kula wala kuhamasika kula chakula kama tusingewekewa ndani yetu tamaa ya chakula, ile tamaa iliyowekwa ndani inatuhamasisha kula chakula, na tunapokula miili yetu inapata faida, na kutimiza lengo la kuendelea kuishi.. Lakini tamaa hiyo inapozidi mipaka inazaa ulafi na ulevi ambao ni dhambi (Soma Luka 21:34, Warumi 13:13, Wagalatia 5:21, na 1Petro 4:3).

Vile vile pia mtu kawekewa tamaa ndani yake ya kimwili kwa jinsia tofauti na yake, tamaa hiyo Mungu kaiweka ndani ya mtu kwa kusudi maalumu na wakati maalumu, kwamba wakati utakapofika mtu aweze kukutana na mke/mume wake na kuzaa watoto, kutimiza Baraka  alizozisema katika Mwanzo 1:28

Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi:”.

Lakini tamaa hiyo inapozidi na kuvuka mipaka kiasi kwamba inampelekea mtu kushindwa kujitawala ndipo anapoanguka katika zinaa na hata zinaaa ya jinsia moja na yake.

Kwahiyo tamaa yoyote ile iwe ya chakula, au ya mwili  kwaasili sio mbaya, ila inapozaa matunda mabaya ndipo inageuka kuwa dhambi..Na ndicho Biblia ilichokimaanisha hapo katika  Yakobo 1:15 kuwa “tamaa ikiisha kuchukua mimba inazaa dhambi”..maana yake katika uasili wake sio dhambi!.. ila inapochochewa kwa njia isiyopaswa ndipo inapozaa dhambi.

Unatazama picha chafu mitandaoni, au unaposoma makala zenye maudhui ya zinaa, au unaposhiriki mijadala yenye maudhui ya zinaa  hapo unaizalia matunda ile tamaa ya mwili ndani yako, na hiyo ni dhambi, kwasababu mwisho wa siku itakupelekea kufanya zinaa au kujichua, au mawazo yako muda wote kutawaliwa na zinaa jambo ambalo biblia imesema kuwa ni machukizo kwa Bwana, moyo uwazayo mabaya (Mithali 6:18).

Biblia inatufundisha kutoyachochea mapenzi..

Wimbo 2: 7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.

Na tamaa nyingine zote ni hivyo hivyo, hatuna budi kuzitawala ili zisizae dhambi, maana mshahara wa dhambi ni Mauti… na tamaa zinazozaa dhambi zote zinatokana na dunia na si MUNGU..

1Yohana 2:16 kuwa tamaa  ya macho na tamaa ya mwili inatokana na dunia na si Mungu

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NI NJIA GANI MTU AITUMIE AWEZE KUSHINDA TAMAA NA VISHAWISHI?

USIWE NA TAMAA YA CHAKULA KINGINE.

USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.

Jiepushe na tamaa ya Mali/kupenda fedha.

Roho ya kukata tamaa ni nini na inatendaje kazi?

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments