Roho ya kukata tamaa ni nini na inatendaje kazi?

Roho ya kukata tamaa ni nini na inatendaje kazi?

Swali: Roho ya kukata tamaa ipoje na inatendaje kazi na inawezaje kumtoka mtu?


“Roho ya kukata tamaa” ni roho inayomwingia mtu na kumfanya asiweze kuendelea mbele Zaidi. Roho hii inapomwingia mtu inamfanya asiwe na nguvu ya kufanya au kutafuta jambo lolote lile lililo zuri. Ndio hapo utaona mtu anakata tamaa ya kuendelea kusubiri jambo Fulani au kuendelea kuomba au kuendelea kutafuta.

Roho hii inasababishwa na “shetani” kwasababu kamwe MUNGU hawezi kumkatisha mtu tamaa kwa jambo lolote jema mtu apangalo kulifanya au kulitafuta. Yeye (Mungu) anasema maneno yafuatayo..

Luka 18:1  “Akawaambia mfano, ya kwamba IMEWAPASA KUMWOMBA MUNGU SIKUZOTE, WALA WASIKATE TAMAA”.

Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

8  kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”

Lakini adui kazi yake ni kukatishata tamaa, aidha kwa njia ya mawazo, ndoto au maneno ya watu.

Zifuatazo ni njia za kushughulika na roho ya kukata tamaa.

   1. MPOKEE YESU

Kama bado hujaokoka, fahamu kuwa wewe ni windo tosha la adui, na moyo wako ni malango ya maskani za roho zote chafu zikiwemo za kukatisha tamaa, hivyo maisha yako yatatawaliwa na kuvunjika moyo na kutokusonga mbele.

     2. SOMA NENO.

Soma sana Neno la MUNGU (Biblia) kwasababu ndani yake limejaa maneno ya Faraja, ambayo yanaweza kukufaa na kukutia nguvu katika nyakati zote utakayopitia za kukatisha tamaa, Kama magonjwa ndiyo yaliyokukatisha tamaa ndani ya biblia ipo mistari mingi ya kutia moyo wa kuendelea mbele.

Kama ni Ndoa ndio iliyokukatisha tamaa, yapo maneno ya faraha na kutia nguvu yahusuyo ndoa ndani ya biblia, kama ni anguko Fulani limetokea na likakukatisha tamaa, ndani ya biblia ipo mistari ya kutia nguvu ya kukunyanyua tena katika hali unayopitia. N.k

    3. MAOMBI

Fanya maombi kila siku, hii utakusaidia kukuweka katika lile joto la kiroho, na hivyo kufunga milango yote ya roho za adui za vitisho na kukatisha tamaa. Ukiwa mwombaji utakuwa katika usalama wa Roho daima.

Kwa njia hizo tatu basi waweza kujifungua na kila kifungo cha kukata tamaa, au kukatishwa tamaa.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?

KWANINI UKATE TAMAA?

Nini maana ya kupiga Kite! Katika biblia.

Maana yake nini, Mwe na hofu wala msitende dhambi? (Zaburi 4:4)

USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments