Swali: Ni hofu gani inazungumziwa katika Zaburi 4:4?
Jibu: Turejee,
Zaburi 4:4 “Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia, 5 Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana”.
Zaburi 4:4 “Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia,
5 Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana”.
Hapa maandiko yanasema “Mwe na hofu WALA msitende dhambi” haisemi “Mwe na hofu ILA msitende dhambi” Kana kwamba hiyo hofu ikizidi sana italeta madhara, hapana bali kinyume chake, inapaswa iwepo nyingi.
Sasa swali ni hofu gani hiyo inayozungumziwa hapo?
Hofu inayozungumziwa hapo si hofu ya kumwogopa mwanadamu, au kumhofu shetani, La! Bali ni hofu ya kumwogopa Mungu (Hofu ya Mungu), ambayo Daudi aliitaja pia katika Zaburi 36:1
Zaburi 36:1 “Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, HAKUNA HOFU YA MUNGU mbele ya macho yake”
Hofu ya Mungu ni ile hali ya mtu kuogopa kuyaasi maneno ya Mungu, hivyo mtu huyo anakuwa anajiweka katika hali ya kujitenga na dhambi siku zote za maisha yake yote. Lakini mtu asiye na hofu ya Mungu anaweza kufanya anayojisikia pasipo kujali kuwa anayoyafanya yanamchukiza Mungu.
Mfano wa watu ambao biblia imewataja hawakuwa na hofu ya Mungu, ni watu wa nchi ya Gerari, ile Ibrahimu aliyoikimbilia.
Mwanzo 20:9 “Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka. 10 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili? 11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini HAPANA HOFU YA MUNGU MAHALI HAPA, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu”
Mwanzo 20:9 “Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka.
10 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili?
11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini HAPANA HOFU YA MUNGU MAHALI HAPA, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu”
Na dunia tunayoishi sasa (mimi na wewe) ni Zaidi ya miji ya Gerari, ni Zaidi ya Sodoma na Gomora, Hofu ya Mungu haipo tena. Na biblia inaonya “tuwe na hofu”, na wala tusitende dhambi.
Je! hofu ya Mungu ipo ndani yako?.. kama hofu ya Mungu ipo ndani yako utaogopa kutenda mabaya, hivyo huwezi kuendelea na ulevi unaoufanya, huwezi kuendelea na rushwa unazokula, huwezi kuendelea na uasherani na uzinzi, huwezi kuendelea la mauaji na kutokusamehe.. ni lazima utajitenga na hayo yote, kwasababu hofu ya Mungu ipo ndani yako.
Bwana atusaidie.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
SIKU YA HOFU YANGU NITAKUTUMAINI WEWE.
BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.
Waoga ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani?(Ufunuo 21:8).
YESU KATIKA USINGIZI WAKE.
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Rudi nyumbani
Print this post