Kama tulivyotangulia kuona kuwa kusoma Neno kunazidisha Ujazo wa Roho Mtakatifu Ndani Yetu..lakini pia ndio Chakula kikuu cha Roho zetu. Bila NENO ni sawa na mwili bila chakula, huawezi kuishi.
Mathayo 4:4
[4]Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
> Kusoma biblia ndiko kunakoweza kukukuza kiroho, (1Petro 2:2,),
> Pia ndipo unapoweza kufanywa upya ufahamu wako (Warumi 12:12).
> Lakini pia Ndani ya biblia kuna unabii wa maisha yako, kuna faraja, Kuna maonyo, kuna mashauri na miongozo (Zaburi 119:105).
Hivyo hakuna Namna mtu atayatenganisha maisha ya wokovu na usomaji Neno.
Sasa unapotaka kuanza kusoma unapaswa ufahamu Kuna usomaji wa aina mbili kuu.
Aina hizi mbili Ni muhimu kuendana nazo. Kuijua biblia yote ni jambo la msingi, kwasababu ili Kuelewa muktadha wa biblia ni lazima kwanza kuzielewa habari mbalimbali zilizo katika biblia.
Hivyo ni lazima Uwe na nidhamu ya kusoma kila siku. Na kama ukifanya Hivyo kwa kusoma sura 6-7 kwa siku, basi ndani ya miezi sita (6), utakuwa umeimaliza biblia yote. Ukimaliza kuisoma rudia tena na tena.
Lakini kusoma kwa muktadha ni kusoma kwa mnyumbuliko, kunahitaji pia mkufunzi Wa kukusaidia kuelewa. Pamoja na utafakariji sana wa Neno, na kwenda taratibu taratibu ili Roho Mtakatifu Akusaidie kuelewa.
1) Hakikisha unakuwa na biblia yako, wewe kama mwanafunzi mpya wa Kristo, yenye agano la kale na lile jipya. Biblia yenye vitabu 66
2) Tenga Muda wa utulivu wa kujisomea kila siku. Ni vema ukawa na mahali pako pa utulivu, ili kuweza kusoma kwa umakini zaidi.
3) Kuwa na daftari Na kalamu, ili Kuandika kila unachojifunza, kwa kumbukumbu zako za baadaye.
4) Omba kwanza kila unapoanza kujisomea biblia ili Mungu Akupe uelewa.
5) Mwisho Hakikisha unakitendea kazi kila unachokisoma.
Kujisomea na wengine pia ni jambo jema la ziada. Uwezavyo kupata rafiki ambaye anapenda biblia, basi kutana naye mara kwa mara, utafakari Naye maandiko. Epuka kampani za watu wasio- na kiu ya Mungu wakati wako huu, tumia muda wako mwingi katika kumtafakari Mungu, ili ukue kiroho kwa haraka, mtoto mchanga huwa ananyonya hata mara saba kwa siku. Kwasababu mwili wake upo katika kukua unahitaji maziwa wakati wote. Vivyo hivyo na wewe hakikisha una muda wa kutosha wa kusoma biblia kila siku.
Vifungu hivi unaweza ukavikariri viwe Kama nanga ya maisha yako ya usomaji Neno.
Zaburi 119:11
[11]Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
Waebrania 4:12
[12]Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Yoshua 1:8
[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Bwana akubariki.
Haya ni mafundisho yanayoweza kukusaidia kupata mwongozo wa usomaji biblia mzuri.
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.
Mtiririko wa vitabu vya biblia kwanini upo vile?
CHAMBUZI ZA VITABU VYA AGANO JIPYA.
NIFANYE NINI ILI NISILALE NINAPOSOMA BIBLIA.
Kwanini kuna tafsiri nyingi za Biblia, na tafsiri ipi ni sahihi?
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
About the author