BIBLIA TAKATIFU.

BIBLIA TAKATIFU.

Biblia takatifu ni kitabu kilichobeba maneno ya Mungu katika mfumo wa maandishi..Kitabu hichi kimebeba taarifa muhimu zote zinazomhusu mwanadamu…biolojia ya mwili wake, mwanzo na mwisho wa milki yake..Biblia takatifu ndio kitabu pekee kinachompa mwanadamu kalenda yake ya miaka inayokuja mbele yake.

Biblia ni kitabu kitakatifu…ndio maana inaitwa “biblia takatifu”… sasa sio karatasi yaliyokiandikia ndio matakatifu, au wino uliotumika kuandikia ndio mtakatifu wala jalada lililotumika…hapana, bali kilicho kitakatifu ni maneno yaliyoandikwa mule ndani.. Kwahiyo kitabu hicho kikitumika kwa akili ya damu na nyama..ya kuamini kwamba makaratasi yale na wino ndio matakatifu hakina manufaa yoyote kwa mwanadamu.

Tukiitumia biblia na kuiweka kifuani mwetu tukiamini kuwa itaondoa matatizo yetu hatutanufaika na chochote, tukiichukua biblia na kwenda kutolea nayo pepo hatutanufaika chochote, tukiichukua biblia na kuiweka kichwani usiku kama mto ili wachawi au mambo mabaya yasitupate hatutaambulia chochote. Ni sawa na mgonjwa anayeumwa kichwa na kuichukua dawa ya panadol na kuiweka kifuani, au kichwani kama mto akiamini itamtibu ugonjwa wake.

Au ni sawa na mtu anayechukua kitabu cha upishi (kinachoelezea hatua ya upishi)..na kukipeleka hicho kitabu jikoni mbele ya masufuria na majiko kimpikie…Unaona kitabu hakiwezi kupika haijalishi kimehakikiwa na mtaala wa nchi, na kupewa daraja la kwanza. Ili kitabu hicho kiwe na manufaa ni sharti aliyenacho akisome, ile elimu iingie kichwani mwake, kwa ile elimu ndipo aitumie kupika.

Vivyo hivyo na biblia takatifu ili iwe na manufaa kwetu, ni lazima tuyasome yale yaliyoandikwa mule ndani, tupate elimu ya kutosha..ndipo ile elimu tuitumie katika kumpendeza Mungu, kumshinda adui, kupata Baraka na mafanikio.

Biblia takatifu ni kitabu cha maarifa, hekima, na mashauri. Hakuna kitabu chochote chenye mashauri bora na hekima zilizo kuu kuliko biblia.

Kwamfano hebu itafakari hii hekima..

Luka 12:23 “Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.

24 Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, na Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!

25 Na yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

26 Basi, ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo, kwa nini kujisumbua kwa ajili ya yale mengine?

27 Yatafakarini maua jinsi yameavyo; hayatendi kazi wala hayasokoti; nami nawaambia ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

28 Basi, ikiwa Mungu huvika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatawatendea ninyi zaidi, enyi wa imani haba?”

Biblia takatifu ndio katiba ya wanadamu. Kwa kutumia katiba mtu anaweza kuhukumiwa na anaweza kupatiwa haki yake. Na kama vile jinsi ilivyo kwamba hakuna mtu aliye juu ya katiba ya nchi..Hata Raisi wa nchi hawezi kuivunja katiba…kadhalika Biblia ni katiba ya wanadamu..hakuna mwanadamu yoyote wala malaika anayeweza kuvuka mipaka ya maneno yaliyoandikwa ndani ya kitabu hicho (yaani biblia takatifu)..Zaidi ya yote hata Mungu mwenyewe hawezi kulivunja Neno lake…Kwamfano alisema hataiangamiza tena dunia kwa maji…haiwezekani hata siku moja akalivunja hilo neno na kuiangamiza dunia kwa gharika…Naam dunia itaadhibiwa kwa kitu kingine kama maandiko yanavyosema katika kitabu cha Petro lakini si kwa maji tena…Na hiyo ni kwasababu analishika Neno lake alilolisema.

Alisema pia yoyote amwaminiye mwanawe mpendwa YESU KRISTO, Ataokoka na hukumu ya milele, na asiyemwamini atahukumiwa…Hilo Neno hawezi kamwe kulibadilisha kwamba..baadaye ageuke na kusema “hapana wote watakaomwamini hawatapata uzima wa milele” wala hawezi kulitangua neno lake alilosema kwamba “wote wasiomwamini watahukumiwa”..Neno lake litabaki palepale..mbingu na nchi zitapita lakini maneno yake yatabaki yale yale.

Biblia takatifu ni maneno ya Mungu yenye ujumbe pia wa maonyo na ahadi. Hakuna kitabu kingine chochote chenye ahadi, kitabu cha fizikia hakina ahadi yoyote, kitabu cha saikolojia hakina ahadi yoyote ndani yake, kitabu cha hisabati hakina ahadi yoyote ile, lakini biblia takatifu imejaa ahadi zilizo thabiti mpaka za vizazi vijavyo vya watoto wetu, mifugo yetu, mali zetu na hata maisha ya ulimwengu ujao.

Bwana atusaidie kulishika Neno lake na kuliheshimu, kwa faida yetu wenyewe hapa duniani na kwa maisha yanayokuja baada ya haya.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?

Kwanini Bwana alirejea Tiro na Sidoni kwa mfano wa Sodoma?

KITABU CHA UZIMA

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments