ELEWA ZAIDI YA WENGINE WANAVYOELEWA.

ELEWA ZAIDI YA WENGINE WANAVYOELEWA.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe sana.. Karibu tujifunze Neno la Mungu wetu mkuu lililo Taa na Mwanga wa njia yetu (Zab. 119:105).

Upo ufunuo mkubwa Musa alioupata uliomfanya awe mpole kuliko watu wote duniani kwa wakati ule, kama maandiko yanavyosema..

Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi”.

Na ufunuo huo ni “KUELEWA ZAIDI YA WENGINE WANAVYOKUWA  WANAELEWA”

Sasa kabla ya kwenda kwa Musa hebu tujifunze kwanza kwa Bwana wetu YESU KRISTO (Mwamba Mgumu).. Bwana wetu maandiko yanasema alikuwa mpole sana (soma Mathayo 11:29 na Mathayo 21:5), kiasi kwamba alitemewa mate hakurudisha, alitukanwa hakujibu, alipigwa hakurudisha mapigo (soma 1Petro 1:23).

Sasa ni kitu gani kilichomfanya awe mpole kiasi kile?, upole ambao ni ngumu kwetu sisi kuwa nao?.. Jibu tunalipata pale kwenye Luka 23:34 aliposema Baba wasamehe kwakuwa hawajui watendalo!.

Luka 23:34 “Yesu akasema, Baba, uwasamehe, KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura”.

Nataka uone hilo Neno “KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO”… Maana yake YESU alikuwa anajua zaidi ya watu walivyokuwa wanajua, alijua wale watu wanafanya mambo wasiyoyajua.. ni kama tu mtoto anayesaidia haya ndani ya nguo yake, anafanya jambo asilolijua ambalo si sahihi, lakini kwasababu wewe unajua zaidi ya yeye ajuavyo, huishii kumkasirikia bali kumsaidia.

Lakini kama usingejua zaidi ya hapo, ungeishia kuona mtoto anafanya makusudi na ni mjinga, na Bwana YESU ndicho alichokiona, aliona wanaomsulubisha si akili zao zinafanya vile, bali wanafanya mambo wasiyoyajua kwamaana kama wangejua ni nani wanayemsulibisha hakika wasingefanya vile, ndivyo maandiko yanavyosema..

1Wakorintho 2:7 “bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;

8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu”.

Ni hivyo hivyo kwa Yuda, wakati wengine wana huzuni ya Bwana kusalitiwa, tayari Bwana alijua sababu za Yuda kumsaliti kuwa hazikuwa akili zake bali ni ili maandiko yatimie, hivyo hiyo haikumfanya Bwana amchukie Yuda au aache ukarimu wake kwake.

Sasa turejee kwa Musa… naye pia siri ya upole wake ni hiyo hiyo!, alikuwa ANAELEWA ZAIDI YA WENGINE WALIVYOKUWA WANAELEWA.

Wakati wana wa Israeli wanamlalamikia na kumnung’unikia Farao na kumwona ni mkatili, Musa alielewa zaidi ya wanavyoelewa wao..

Wakati wengine wanamwona Farao ni Mgumu, lakini Musa alielewa kuwa ule ugumu wa moyo wa Farao ni Mungu ndiye aliyeuweka ndani yake, hivyo Farao alikuwa hafanyi yale kwa akili zake.. kwahiyo Musa hakuchanganywa na kiburi cha Farao, kwasababu alikuwa anaelewa zaidi ya wengine wanavyoelewa..

Kutoka 4:1 “Bwana akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; LAKINI NITAUFANYA MGUMU MOYO WAKE, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao”.

Na hiyo ikamfanya Musa awe mpole kuliko wengine wote kwasababu alijua kila kitu kipo chini ya uongozo wa Mungu.

Vivyo hivyo na wewe na mimi, ni lazima tuelewe zaidi ya wengine wanavyoelewa ili tupate utulivu, wakati mwingine huwezi kupata utulivu usipojua sababu ya mambo, si kila tukio baya linalotokea mbele yako ni shetani, mengine Mungu anayaleta kwasababu maalumu, kinachohitajika ni utulivu na kumngoja Bwana.

Si kila mtu anayekukataa kapewa huo moyo na shetani, wengine ni Mungu kaifanya mioyo yao hivyo, ili Mungu baadae aonyeshe uweza wake wote kwako, na umtukuze!..unaweza ukajaribu kufanya kila kitu kizuri na hata ukaonyesha wema wote bado usipate kibali, hiyo haina tafsiri kwamba kuna shida kwako, hata Musa alitoa ishara tisa mbele ya Farao lakini hazikuzaa matunda..ila mwisho wake ulikuwa mkubwa.

Vile vile nawe pia kabla hujafikiria kupaniki kwa hali yoyote unayokutana nayo mbele yako, hebu tuliza kwanza akili kumwomba Mungu akufunulie sababu.. Hali nyingine za misukosuko hazitoki kwa shetani, bali ni Mungu anayezileta kwa makusudi yake Mema, kwasababu kamwe Mungu hapendi kuwatesa wanadamu, lakini anayaruhusu mengine ili yalete ushuhuda mkubwa hapo mbeleni.

Tafakari vipi kama Farao angetii tu kwa lile pigo la kwanza, leo tusingemjua Mungu katika uweza ule wote, vipi kama Ayubu asingepitia yale yote, leo tusingemjua Mungu kama ni mwokozi anayerudisha vyote ambavyo vimepotea kabisa..kwahiyo ni kutulia tu na kumwomba Mungu uelewa wa kina wa yanayoendelea!.

Na ukipata uelewa wa kutosha wa yanayoendelea, au yaliyotokea zaidi ya ulivyokuwa unaelewa, au watu wanavyoelewa, utakuwa mpole kuliko watu wote, utakuwa na ujasiri kuliko watu wote, utakuwa mwenye nguvu kuliko watu wote, pasipo kujali hali zinazoendelea.

Bwana atusaidie tupate kuelewa ziaid ya tunavyoelewa sasa.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je! Petro na wenzie walitambuaje kuwa wale walikuwa ni Musa na Eliya?

Huyu Mkeni shemeji yake Musa alikuwa ni mtu wa namna gani? (Waamuzi 1:16)

Kiti cha Musa ni kipi? (Mathayo 23:2)

TUKIO LA MUSA NA ELIYA KUMTOKEA BWANA, LIMEBEBA UJUMBE GANI?

Kwanini Musa amtake Hobabu na tayari kulikuwa na Wingu linalowaongoza?

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments