Waebrania 12:29
[29]maana Mungu wetu ni moto ulao.
Mungu huitwa moto, lakini si moto tu bali moto ulao, maana yake si ule wa kuunguza tu, bali Ule wa kulamba kila kitu, kutafuna Na kutowesha kabisa
Mfano wake ni kama ule ulioshuka juu ya madhabahu Aliyoijenga Eliya, uliposhuka, juu yake haukuchagua maji, wala kuni, wala sadaka..mahali pale palimezwa kila kitu…(1Wafalme 18:38)
Tofauti na mioto Mingine ambayo itaivisha tu kitu, au kugeuza umbile n.k. moto huu haubadilishi umbile Kama hii mioto mingine tuliyonayo…ambayo ikipita Juu ya chuma Haiwezi kuila yote, bali huiyeyusha Tu na kuibadili umbile, huo wa Mungu hulamba Vyote bila kubagua…
Huu ni moto wa rohoni sio mwilini.. ukijazwa huu, basi fahamu hakuna chochote ambacho hakifai kisichoungua….ugusapo popote..huharibu kabisa Kabisa kazi za shetani, ukaapo ndani yako huchoma kabisa kabisa mambo maovu.
Hivyo Bwana ametutaka kama watoto wake aliotuzaa tujawe na moto huu ndani yetu.. na namna ya kuupokea..ameeleza katika vifungu vifuatavyo;
Isaya 33:14
[14]…. Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele? [15]Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung’utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.
[14]…. Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?
[15]Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung’utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.
Umeona ni nani Awezaye kukaa na moto ulao? Kumbe si wote…bali ni wenye sifa hizo zilizotajwa..
Maana yake, kwa kauli ya ujumla ni yule yeye atafutaye kuishi maisha matakatifu na ya haki.
Hii ndio mbio yetu wote…
Nguvu ya ukristo baada ya kuokoka ni utakatifu. Ndio moto wetu ulao.
Bwana akubariki.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Kutawa ni nini? Sawasa na Luka 1:24
Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.
Yohana aliwatiaje waasi akili za wenye haki? (Luka 1:17)
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ