Je kuna walioandikiwa mabaya  na wengine mema?

Je kuna walioandikiwa mabaya  na wengine mema?

Swali: Unakuta mtu anapitia tatizo fulani, halafu anasema.. ndio nimeandikiwa hivyo! Na siwezi kubadilisha.. sasa je mtu anaweza kuwa ameandikiwa mabaya yampate na mwingine mema?


Jibu:  Kifungu cha Biblia kinachosapoti kuwa mtu anaweza kuwa ameandikiwa mabaya au mema ni kutoka katika kitabu cha Yeremia..

Yeremia 15:2 “Kisha itakuwa, hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, Bwana asema hivi, WALIOANDIKIWA KUFA, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; AU KUFA KWA NJAA, WATAKUFA KWA NJAA, au kutekwa nyara, watakuwa mateka”.

Kwa haraka andiko hilo laweza kueleweka kwamba wapo watu walioandikwa na MUNGU matatizo tangu mwanzo, lakini kiuhalisia haiko hivo.. hakuna mtu aliyeandikiwa na MUNGU matatizo, au shida..

Sasa kama hivyo ndivyo, nini maana ya andiko hilo ya kwamba “waliondikiwa kufa watakufa? (Yeremia 15:2)”

Mantiki ya “kuandikiwa hapo” inarejea sheria za Mungu huko nyuma.. kwamba iliandikwa “Mtu asiyeishi kwa sheria za Mungu atadhibiwa kwa sheria”… Kwamfano iliandikwa hivi katika Kumbukumbu 28:15-18..

Kumbukumbu 28:15 “Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.

16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.

17 Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.

18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako”.

Sasa kulingana na andiko hilo, mtu Yule ambaye ataacha kusikiliza sauti ya Bwana na atafanya mabaya… basi maandiko hayo ya laana yatampata, na hapo ni sawa na kusema kwamba “ameandikiwa laana”

Lakini si kwamba Mungu anamchagua mtu na kumwandikia laana na mwingine anamchagua na kumwandikia Baraka!… La!..Bali laana zake na Baraka zake zinakuja juu ya mtu kwasababu ya matendo ya mtu.

Kwahiyo mtu aliyekufa kwa upanga huwenda ni kwasababu aliua kwa upanga, na hivyo andiko hili ndio aliloandikiwa na limetimia kwake..

Ufunuo 13:10 “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga….”

Na makosa mengine yote ni hivyo hivyo, yameshaandikiwa adhabu yake.. kwahiyo mtu akiyatenda atakuwa anapokea malipo ya yaliyoandikwa na kuichukua hiyo nafasi.

Bwana atusaidie, tusitimize maandiko ya Laana, bali tutimize maandiko ya Baraka ili tuwe miongoni mwa waliondikiwa Baraka.

Je umempokea YESU, Umebatizwa kwa Roho Mtakatifu?.. kama bado unasubiri nini?…fahamu ya kuwa unyakuo wa kanisa umekaribia sana na siku yoyote parapanda ya mwisho inalia na wafu wanafufuliwa.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UVUKISHE MIPAKA UPENDO WAKO.

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

FAIDA NYINGINE YA MAOMBI YA KUSHUKURU.

ILI TUONEKANE SAFI MBELE ZA MUNGU TUFANYE NINI?

LINDA CHEMCHEMI YA MOYO WAKO.

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply