Ni umeme gani Bwana anaouzungumzia katika (Mathayo 24:27)?

Ni umeme gani Bwana anaouzungumzia katika (Mathayo 24:27)?

Swali: Katika Mathayo 24:27, tunaona “UMEME” ukitajwa, Je kipindi cha Bwana YESU umeme ulikuwepo?


Jibu:  Turejee..

Mathayo 24:27 “Kwa maana kama vile UMEME utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu”.

Umeme unaozungumziwa hapo ni ule “MWANGA WA RADI” unaoonekana nyakati za Mvua… Kwaasili “Radi” ni “Umeme” na si Moto. Na tangu Uumbaji Radi zipo,

Ayubu 28:26 “Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa UMEME WA RADI”.

Soma pia Ayubu 37:15, Zaburi 77:18, Zaburi 135:7, Yeremia 10:13, Yeremia 51:6, Danieli 10:6 na Nahumu 2:4 na Luka 10:18.

kwahiyo hapo maandiko yamemaanisha kuwa kama vile Radi imulikavyo kutoka mashariki hata magharibi ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.

Na kwanini Umeme umetumika kufunua ujio wa YESU?.. Ni kwasababu ya Nguvu ya Umeme, na kasi ya Umeme.. Kikawaida Radi huwa inapiga sehemu ya juu iliyoinuka nan a inaweza kupasua mti wa Mbuyu ulio mkubwa vipande viwili chini ya dakika moja..

Na YESU KRISTO atarudi kwa nguvu hizo hizo, na kupakanyaga mahali pa juu pa dunia palipoinuka (Amosi 4:13)

Isaya 22:5 “Kwa maana siku ya kutaabika, SIKU YA KUKANYAGWA, SIKU YA FUJO INAKUJA, itokayo kwa Bwana, Bwana wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima”.

Je umempokea YESU?.. na kumfanya Bwana na Mwokozi wa maisha yako? Na kuishi maisha matakatifu ya kumpendeza yeye?.. Kama bado unasubiri nini?.. Ni heri ukayasalimisha maisha yako kwa YESU leo, kwamaana siku hizi tuishizo ni siku za hatari na dakika yoyote ule mwisho unafika.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

Kwa namna gani mauti hufanya kazi ndani yetu na uzima kwa wengine? (2Wakorintho 4:12).

FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply