Ipi tofauti ya “Majibu” ya Maombi na “Majaribu”.

Ipi tofauti ya “Majibu” ya Maombi na “Majaribu”.

Swali: Je nikiomba kazi kwa mwaka mmoja na ikatokea fursa ambayo inanitaka nitoe rushwa kidogo ili niingie kazini, je hilo ni Jibu la Maombi yangu, au ni jaribu?


Jibu: Hilo si jibu la Maombi, bali ni “Jaribu” linaloletwa na ibilisi mbele yako. Majibu ya Maombi hayana njia za mkato, yanakuwa yamenyooka na yenye kibali.

Lakini inapotokea tunaomba jambo kwa Mungu atutendee, halafu inatokea fursa nyingine iliyo kinyume na Neno la MUNGU, hilo ni jaribu na tunapaswa tulishindwe.

Mfano mwingine ni pale mtu ameomba hitaji fulani kwa Mungu labda fedha ya kodi, halafu inatokea fursa ya wizi, utakaokamilisha kile kiasi.. sasa hiyo fursa si kutoka kwa MUNGU hata kama inakupa wepesi mkubwa wa kupata kile kiasi, bali ni Jaribu la maombi yako, na ni lazima kulishinda.

Au unaomba mume halafu anakuja Mume wa Mtu kutaka kukuoa, hayo sio majibu ya maombi bali ni majaribu..

Na yapo mambo mengine mengi,  yanayokuja kwa sura ya Majibu ya Maombi, lakini nyuma yake ni Majaribu ya maombi.

Sasa ni kwa namna gani tunaweza kutofautisha Majibu na Majaribu?.

Hakuna njia nyingine zaidi ya “KULIJUA NENO LA MUNGU”..Na hatulijui Neno la Mungu kwa kukariri mistari ya Biblia, au kuelezewa bali kwa “KUJIFUNZA BIBLIA”.

Huwezi kujua dhambi ni nini kama hauijui Biblia..

Warumi 7:7 “Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani”.

Pia hatutaweza kuyajua majaribu ya ibilisi kama hatutalijua Neno la MUNGU ndani ya Biblia takatifu.

Weka desturi za kusoma Biblia kwa kujifunza, usiwekeze tu peke yake katika Maombi na ukaliacha Neno la Mungu pembeni, ukiwa mtu wa namna hiyo, ibilisi atakuletea majaribu ukidhani ndio majibu ya maombi yako, na kufanya mfungo wako au maombi yako kuwa si bure.

Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NYAKATI TOFAUTI- TOFAUTI ZA UPENDO.

MAJARIBU 10 WANA WA ISRAELI WALIYOMJARIBU MUNGU.

NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?

KISIMA BADO KINA MAJI, KIFUKUE TENA.

FAIDA NYINGINE YA MAOMBI YA KUSHUKURU.

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply