Biblia inatuambia kuwa sauti ya Bwana YESU ni kama sauti ya maji mengi..
Ufunuo 14:2 “Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, KAMA SAUTI YA MAJI MENGI, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao”.
Sasa maji mengi kazi yake ni ipi?..
1. KUONDOA UCHAFU.
Maji mengi yenye nguvu, yanagharikisha uchafu, na kutakasa kila mabaya ndani ya mtu.
Isaya 28:2 “Tazama, Bwana ana mmoja aliye hodari, mwenye nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe, tufani iharibuyo, kama DHORUBA YA MAJI MENGI yafurikayo, ndivyo atakavyotupa chini kwa mkono”
Kwahiyo sauti ya Bwana/maneno ya Bwana YESU yakisikiwa na kuaminiwa na kutendewa kazi yanagharikisha na kusafisha mabaya yote ndani ya maisha ya mtu na pia matatizo na maradhi.
Zaburi 29:3 “Sauti ya BWANA i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi”.
2. KUKATA KIU.
Maji mengi yanakata kiu.
Zaburi 78:15 “Akapasua miamba jangwani; Akawanywesha maji mengi kama maji ya vilindi”.
Kiu ya kupata furaha, amani, ulinzi, utulivu na mengineyo mema kupitia sauti ya Bwana ya maji mengi, kiu hiyo inakatika, mtu ataanza kupata amani na furaha na hali ya kuridhika akiwa ndani ya YESU.
Pia kiu ya kufanya dhambi inaondolewa ndani, mtu huyo anajikuta hatamani tena kufanya dhambi.
Kwa YESU kuna maji tele! Yatakayogharikisha matatizo yako yote na pia yatakayokaya kiu yako yote,
YESU yupo hai na anakuita leo.
Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ