Kwanini Sadaka ya Kaini ilikataliwa? (Mwanzo 4:5).

Kwanini Sadaka ya Kaini ilikataliwa? (Mwanzo 4:5).

Swali: Kwanini sadaka ya Kaini ya Mazao ilikataliwa na ile ya Habili ya wanyama ilikubaliwa? Je ni kwamba “wanyama” ni bora kuliko “mazao” mbele za Mungu?


Jibu: Turejee,

Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;

5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”.

Sababu ya sadaka  ya Kaini kukataliwa si kwasababu Mungu anapendezwa sana na wanyama kuliko mazao.. LA! Zaidi sana Mazao yanaweza kuwa bora kuliko wanyama kwasababu hayahusishi umwagaji wa damu.

Lakini sababu kuu ya Sadaka ya Kaini kukataliwa ni hiyo tunayoisoma katika mstari wa  3 na wa 4..

“Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta WAZAO WA KWANZA wa wanyama wake na SEHEMU ZILIZONONA za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;”

Habili alileta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona… Lakini Kaini hakupeleka sehemu za kwanza za mazao yake!..bali alipeleka sehemu dhaifu,  kama ni mahindi pengine alipeleka yale yaliyoharibika haribika, kama ni matikiti alipeleka yale yaliokaribia kuoza! N.k..na zile njema na nzuri aliona zinamfaa yeye na si Mungu anayempa pumzi, na uhai na maisha.

Hivyo alimfanya Mungu wapili katika mali zake, na Mungu naye akamfanya wa pili mbele ya ndugu yake Habili.

Lakini Mungu ni wa upendo, huwenda alifanya vile kwa kukosa maarifa.. hivyo alimwonya na kumfundisha njia iliyobora ya kutoa sadaka ili sadaka yake ikubaliwe kama ya nduguye, lakini kwa kiburi alishupaza shingo, na akaenda kumwua ndugu yake, ikawa dhambi kubwa sana kwake.

Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.

4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;

5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.

6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?

7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.

9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? “

Ni jambo gani tunajifunza hapo?

Jambo kuu tunalojifunza ni kuwa Mungu anaziangalia sadaka zetu, na kupitia hizo anatuhukumu nazo!.. Maandiko yanasema “hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake utakapokuwepo (Mathayo 6:21)”.. Kama hazina yako ya kwanza haipo kwa Mungu, na Moyo wako hauwezi kuwa kwa Mungu, na ndicho kilichokuwa kwa Kaini.. Hazina yake kamilifu haikuwa kwa Mungu ndio maana hata Moyo wake haukumwelekea Mungu baada ya pale.

Lakini kama sehemu ya kwanza ya Hazina yako (sadaka) ipo kwa Mungu hata moyo wako utakuwa kwa Mungu..

Na kama unataka kujipima kama moyo wako kweli upo kwa Mungu “jiangalie utoaji wako”..(Hicho ndio kipimo kirahisi sana cha kujitambua wewe ni mtu wa namna gani).. Kwasababu hiyo basi ni dhambi kubwa sana kukwepa matoleo, haihitaji elimu kubwa kufahamu hilo….mtolee Bwana Zaka, mtolee Bwana sehemu zilizonona wala usimwibie, na moyo wako utakuwa kwake na utabarikiwa pia.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?

Biblia inaposema Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, Inamaana gani?

SISI NI WINDO BORA SANA, LA DHAMBI.

DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?

SADAKA INAHARIBU NGUVU ZA MADHABAHU ZA MASHETANI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments